Nafasi Ya Matangazo

July 16, 2013

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO wanatarajia kuzindua radio jamii katika wilaya ya Karagwe mkoani Bukoba mwishoni mwa wiki hii
 
Uzinduzi huo unafatia ushirikiano kati ya Airtel na UNESCO katika mradi wa kusadia jamii na kufikisha mawasiliano ya radio sehemu ambazo zina changamoto za huduma za mawasiliano ya radio
 
Akiongea kuhusu uzinduzi huo ya Airtel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema  “ Mradi huu wa radio za jamii tunaufanya kwa kushirikiana na UNESCO kwa lengo la kuendeleza na kuboresha huduma za mawasiliano na kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani wa maeneo ya vijijini.
 
Tumejipanga kufanya uzinduzi wa ushirikiano wetu na UNESCO na Radio ya FADECO Karagwe utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 19 julai 2013
 
Mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Bukoba LutenFabian Masawe , pamoja na yeye tutakuwa na viongozi mbalimbali wa serikali watakaohuduria sherehe za uzinduzi huo
 
Tunaamii kwa kupitia radio hizi jamii itabadilika na kupata elimu zitakazosaidia kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wananchi wengi wana pata habari mbalimbali zikiwemo za kibiashara, uchumi, kijamii na kisiasa.
 
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin alisema “tunayo miradi mingi ya kusaidia jamii kujikwamua na hali ngumu za uchumi, kupata elimu bora, uongozi bora , kuachana na mila potofu na mengine mengi.  kwa kupitia mradi huu wa Radio tunaoshirikiana na wenzetu wa Airtel tumeshaona matunda na mafanikio mengi mpaka sasa, lengo letu ni kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo za kuwapata wananchi habari za ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na sehemu nyingine za nchi na Dunia.
 
Akiongea kuhusu uzinduzi wa Radio jamii Karagwe Mkurugenzi wa Radio ya FADECO Bw Joseph Sekiku alisema “Mpaka sasa vifaa na mitambo ya mawasiliano ya kisasa imeshafungwa na tuko katika hatua ya majaribio ambapo tumeshuhudia ufanisi mkubwa zaidi kulinganisha na awali kwani tumeweza kutanua wigo na kufikia vijiji vingi zaidi”.
 
nawashukuru sana Airtel na UNESCO kwa kutufikia na kuwawezesha kuendesha radio yetu kwa ufanisi zaidi. Radio ya FADECO ilizinduliwa toka mwaka 2007  na kuanza  kurusha matangazo yetu rasmi kwa vijiji vya karibu, changamoto tuliyokuwa nayo ni pamoja na kurusha matangazo yetu katika vijiji vilivyo mbali zaidi kutoka hapa radioni. Kwa kupitia mradi huu tumeweaza kuona mfanikio makubwa tayari, 
 
“Tunagemea kuzindua rasmi ushirikiano wetu na UNESCO pamoja na Airtel siku Ijumaa hapa Karagwe. Nachukua fulsa kuwaalika wananchi wadau wa sekta za mawasiliano, viongozi mbalimbali kuhudhuria halfa hii ya uzinduzi na kusherehekea pamoja nasi mafanikio haya” aliongeza Sekiku
 
Mradi wa radio jamii umeanzishwa mwaka jana 2012 radio zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi zitafaidika na mradi huu kama ilivyo katika Radio hii ya FADECO iliyopo wilaya ya Karagwe Bukoba
Posted by MROKI On Tuesday, July 16, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo