Nafasi Ya Matangazo

April 03, 2013

Na Father Kidevu Blog, Itilima-Simiyu
Wanawake watatu wakazi wa Kijiji cha Kashishi, Kata ya Nzanzui Tarafa ya Kinang'weli, Wilayani Itilima Mkoani Simiyu watalazimika kukihama Kijiji chao baada ya wananchi wenzao kijijini hapo kuwatuhumu kwa Imani za Kishirikina.

Akizungumza na Blog hii, Katibu Tarafa wa Kinang'weli, Sheila Kikula, amesema wananchi hao hivi sasa wapo chini ya uangalizi wa Polisi na bado maamuzi hajafikiwa rasmi kuwa ni wapi wahamie na Polisi wamewapeleka kuchukua vyombo vyao.

Taarifa zilizotolewa zinasema kuwa chanzo cha akina mama hao kushambuliwa kwa mijel;edi na wananchi kasha kuwatishia kuwapotezea uhai ni kuugua kwa kijana mmoja kijijini hapo aliyedai kulogwa na akina mama hao.

Mara baada ya taarifa hizo kusambaa siku ya Juma pili ndipo wakavamiwa na kushambuliwa lakini kijana huyo alipelekwa Hospityali ambako amelazwa hadi hivi sasa akisumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.

Kikula amesema akina mama aho ambao ni vikongwe wameshambuliwa vibaya kwa fimbo na wananchi wenzao jambo ambalo limepelekea kuvimba mwili na kuwa na majeraha ya hapa na pale.

Aidha Katibu Tarafa huyo amesema wananchi hawana budi kuacha vitendo vya kikatili na kujichulia sheria Mkononi dhidi ya watuhumiwa wowote bali watoe taarifa Polisi na kushughulikiwa kisheria.

Pia ametoa wito kwa Viongozi wa Dini mbalimbali nchini kufika eneo hilo na kutoa huduma za kiroho kwani Wimbi la imani hizo za kishirikina ambalo kiserikali haliaminiki ni kukosekana kwa huduma za kiroho miongoni mwa Jamii.

“Ipo haja kwa viongozi wa dini na madhehebu kufika hapa na kuanzisha makanisa na Misikiti ili watu wawe na hofu ya Mungu na kuacha imani ambazo hazimpendezi Mungu”, alisema Kikula.
Posted by MROKI On Wednesday, April 03, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo