Nafasi Ya Matangazo

April 04, 2013

 Watangazaji wa kipindi cha Guinness Football Challenge Larry Asego(kulia) na Flavia Tumsiime(kushoto).
 Washindi wa kipindi cha Tatu cha Guinness Football Challenge,Kenneth Kamau(kulia) na Wills Ogutu (kushoto) wote wanatoka Nairobi Kenya, katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego na Flavia Tumsiime.
*******       ********
Katika sehemu ya tatu jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalionesha ni jinsi gani utulivu unavyosaidia katika mashindano ambapo timu kutoka Kenya ilifanikiwa kuzitoa timu nyingine za Tanzania, Uganda na timu nyingine kutoka Kenya . 

Kenneth Kamau na Wills Ogutu walishinda katika mikwaju ya penati na kufikia hatua ya mwisho katika ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walifanikiwa kulenga matundu manne na kupata fedha za kimarekani dola 5,500. Kwa bahati mbaya walishindwa kulenga tundu la mwisho na hivyo kupelekea kupoteza dola 2,500 na kuondoka na fedha za kimarekani taslimu dola 3,000.

Kenneth na Wills wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .

Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
Posted by MROKI On Thursday, April 04, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo