Nafasi Ya Matangazo

April 17, 2013



Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal jana kabla ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa  Pamoja wa Wanasayansi watafiti Afrika alipata fursa ya kutembelea mabanda ya Monyesho yaliyopo katika Viwanja vya Snow Crest Hotel jijini Arusha.

Maonesho hayo yanafanyika kwa siku nne sambamba na Mkutano huo.Pichani ni Makamu wa Rais akiangalia vimelea vya magonjwa kwa kutumia darubini.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kushoto) akiteta jambo na Wabunge Steven Ngonyani 'Maji Marefu' na Cecilia Paresso.
 Makamu wa Rais kabla ya kuingia katika Mabanda hayo alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Afya na Usatawi wa jamii pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR).
 Makamu wa Rais akipata maelezo ya namna ya Chujio la Maji linalofanyiwa utafiti na NIMR linavyofanya kazi ya kuchuja maji na kuwa salama kwa kunywa. Pindi utafiti huu utakapokamilika wananchi wataweza kunywa maji safi na salama majumbani mwao.
 Akiendelea kupata Maelezo...
 Makamu wa Rais alijitahidi kupita kila Banda na lupata maelezo ya kina ya Wahusika.
 Chuo Kikuu cha Muhumimbuli nacho kipo katika maonesho hayo.
 Moja ya Makampuni yanayouza vifaa vya Mahospitalini nayo yalikuwepo katika maonesho hayo mjini Arusha.
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipita katika banda la Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS)
 Makamu wa Rais akipata maelezo ndani ya Banda la Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).
 Makamu wa Rais akiwa banda la OHCEA.
 David Mbulimi kutoka Taasisi ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Ifakara, akitoa Maelezo ya taasisi hiyo kwa Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Seif Rashid.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akipita katika banda la Mamlaka ya Chalula na Dawa Tanzania (TFD),
Posted by MROKI On Wednesday, April 17, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo