Nafasi Ya Matangazo

April 24, 2013

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina, akizungumza na waanbdishi wa habari Makoa Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam juu ya mchakato wa Matembezio ya Hisani ya Step Ahead mwaka huu ambayo yatafanyika Juni 8, 2013 na yatakuwa ya Kilometa 5 ambapo Mgeni Rasmni anataraji kuwa Dk. Asha-Rose Migiro. Pamoja nae ni Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Susan Boon.
Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dr, Festus Ilako (kulia) akizungumzia ushiriki wa Shirika hilo katika kufanikisha matembezi hayo  ya Hisani ya Step Ahead mwaka huu ambayo yatafanyika Juni 8, 2013 na yatakuwa ya Kilometa 5 ambapo Mgeni Rasmni anataraji kuwa Dk. Asha-Rose Migiro. Pamoja nae ni Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Susan Boon (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe akifdafanua jambo kwa wanahabari juu ya matembezi hayo ya Hisani. Wengine katika picha ni Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Susan Boon (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina.
 Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini Tanzania na Afrika Mashariki wakisikiliza kwa makaini uzinduzi wa matembezi hayo ya hisani ambapo nawao wamehimizwa kushiriki ili kuchangia Matibabu na afya ya mama na mtoto  nchini.
 ****   ****
Kila mwaka Benki ya Barclays inaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step Ahead Walk. Mchakato huu umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006 na Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo  fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.

Matembezi haya ya hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu  wa benki  ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii.  Tangu ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga– ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.

Akiongea katika vyombo vya habari leo, Ndugu, Kihara Maina, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania amesema, tukio hili rasmi itafanyika tarehe 8 juni, 2013 katika hoteli ya Golden Tulip na litahusisha matemebzi ya hisani ya kilomita tano (5) na kila mtu katika jamii anakaribishwa kushiriki. Tiketi zitauzwa kwa shilingi za kitanzania 5000 na zitapatika katika kila tawi la Benki ya Barclays kuanzia tarehe 29 Aprili, 2013

Susan Boon, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT amesema “msaada huu ambao  CCBRT wanaupokea kutoka Benki ya Barclays ni wa thamani sana ambapo tunafanya  kazi ili kufikia malengo ya Tanzania ambapo jamii itajiwezesha kupaha huduma bora na salama hasa kwa walemavu wa viungo na pia itawafikia wakinamama wote na kuhakikishia usalama wao kwenye  huduma ya  afya ya uzazi na watoto wachanga inafanikiwa. Mkakati huu wa benki ya Barclays Step Ahead utasaidia pia katika kukinga mapungufu ya mtindio wa ubongo na fistula hapa Tanzania, na vile vile kuhakikisha kwamba wale waliopata mapungufu wakati wa kuzaliwa wanapata matibabu  katika sehemu za viungo vyao haraka iwezekanavyo.

Pia kwa kushirikiana na taasisi zetu za hapa nchini CCBRT na benki ya Barclays Tanzania tunakusudia kuwa mfano mzuri na muhimu katika jamii inayotuzunguka na tunafutrahia sana kuwa chachu ya msaada katika jamii yetu inayotuzunguka ya Tanzania.”

Akiongea pia na waandishi wa habari katika mkutano na vyombo vya habari, Dr, Festus Ilako Mkurugenzi wa AMREF Tanzania amesema “Msaada na mkakati huu wa benki ya Barclays Tanzania kwa AMREF ni wa kila wakati, na kwa pamoja tunaweza tukaibadilisha jamii kutoka ilipo katika masuala ya afya kwa wakina mama na watoto, hivyo kuitengenezea jamii uelewa na ustadi katika kusimamia afya njema na kuvunja marudio rudio  ya ufukara katika afya na umaskini.

Kampeni hii kutoka benki ya Barclays ijulikanayo kama Step Ahead itasaidia kuelimisha wakunga na wazalishaji katika wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na kuwawezesha wakina mama wajawazito kujifungua katika mikono ya salama ya wafanyakazi waliofuzu katika Nyanja ya afya hivyo kupunguza uchangiaji wa vifo visivyo lazima na ulemavu wa viungo kwa mama na watoto chini ya miaka mitano.  Ushirika huu baina ya Barclays na AMREF ni mfumo mpya  ambayo utawezesha jamii kupata ubora na unafuu katika masuala ya kiafya.

Mwaka 2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kuchangisha shilingi za kitanzania milioni 150 kutokana na  mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili. Mwaka huu lengo ni kuchangisha zaidi ya marambili ya shilingi milioni 150 kutoka kwenye matoleo ya washirika muhimu na washiriki wengine katika jamii.

Fedha zitakazochangishwa mwaka huu zitakwenda kusaidia katika masuala ya uzazi na afya ya watoto kama ifuatavyo:-
1. Mafunzo kwa wakunga wa uzazi
2. Matibabu ya Fistula
3.Upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu unaosababishwa na uzazi

Step Ahead Walk 2013 itaweza kufanikiwa tu kama itawezeshwa na kila mshiriki na jamii nzima ya kitanzania kwa ujumla. Kwa sababu hiyo basi tujiunge wote ili tuweze kufanya badiliko katika masuala ya afya kwa ujumla hapa Tanzania hususani masuala ya uzazi na afya ya watoto.
Posted by MROKI On Wednesday, April 24, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo