Nafasi Ya Matangazo

April 11, 2013


Mkuu wa Usambazaji Musa Kito akiwa ameshikilia Sanduku la Dhahabu, wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Maisha Bomba na Baclays ndani ya Sanduku kla Zahabu uliofanyika leo katika Ofisi za beki hiyo tawi la Morocco jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa kitengo cha biashara cha benki ya Barclays Tanzania, Samuel Mkuyu (kulia) akiwa pamoja na Meneja Masoko wa Baclays, Rahma Ngassa (kushoto), Mkuu wa Usambazaji Musa Kito na Afisa Mawasiliano, Lilian Machera wakiwa wameshikilia Sanduku la Dhahabu, wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Maisha Bomba na Baclays ndani ya Sanduku kla Zahabu uliofanyika leo katika Ofisi za beki hiyo tawi la Morocco jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Baclays Bank tawi la Morocco jijini Dar es Salaam wakiwa katika uzinduzi huo.
********      **********


Barclays Tanzania leo imetangaza rasmi uzinduzi wa kampeni yake ya Sanduku la Dhahabu kwa wateja wake muhimu wa sasa na wale wanaolengwa kwa baadaye.

Barclays itaendesha kampeni hii muhimu ambayo itawapa wateja wao muhimu fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3). Ukiweka pesa zako benki na ukaweza kubakisha salio lililokusudiwa, wewe ukiwa kama mteja wetu wa sasa na hata yule mpya utaweza kuingia kwenye droo ambapo wateja 10 watajinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla atajinyakulia zawadi ya shilingi millioni kumi za kitanzania (Tsh 10,000,000). Promosheni hii inaanza leo hii tarehe 11 Aprili 2013 hadi tarehe 30 Juni 2013 (3)

Akiongea na waandishi wa habari leo hii, Kaimu Mkuu wa kitengo cha biashara cha benki ya Barclays Tanzania bwana, Samuel Mkuyu  amesemashindano hili liko wazi kwa wale wateja wapya na wa zamani wenye akaunti za binafsi ambao wanahifadhi pesa zao na benki yetu hapa tanzania kwenye akaunti ya Kuweka”.

Akiongezea wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni hii ni wale tu wenye akaunti za Hundi na Akiba, na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye akaunti mpaka lifikie shilingi laki tano za kitanzania (Tsh 500,000), na salio hili libakie kwenye akaunti bila kupungua ndani ya mwezi wa shindano.

Kwa wale wateja wapya wanaweza wakaweka shilingi laki tano kwenye akaunti zao bila kuzipunguza na wakaingia kwenye shindano la mwezi walioweka pesa zao. Wateja wetu wote wa sasa na wapya wataweza kuingia na kujishindia zaidi ya mara moja iwapo wataongeza ziada ya shilingi laki tano (Tsh.500,000 ) ndani ya mwezi husika.

 Zawadi kubwa na ya jumla itatolewa kwenye sanduku la dhahabu, na pia washindi wote wa mwezi wa sita watapata nafasi ya kuchagua sanduku la dhahabu wanalolipenda kila mmoja na ndani yake kutakuwa na zawadi mbalimbali

  • 2 iPad mbili (2)vocha tano (5) za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya shilingi laki mbili za kitanzania (Ths 200,000) kila moja, mashine za kufulia nguo mbili (2), na cinema moja (1) ya ndani.
  • Vocha za manunuzi za Shilingi 200,000 kila moja.
  • Mshine za kufulia mbili (2)
  • . Shindano hili litafanyika kila wiki ya kwanza ya kila mwezi na kuzingatia walioingia kwenye shindano mwezi uliotangulia.
Posted by MROKI On Thursday, April 11, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo