Nafasi Ya Matangazo

February 18, 2013


FAMILIA  ya Marehemu Mathew Ndesamburo Chao wa Mazimbu Morogoro, inasikitika kuwatangazia Msiba wa Binti yao Mpendwa Grace Chao kilichotokea leo asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

Mipango ya Mazishi kwa sasa inafanyika nyumbani kwa dada wa Marehemu Yopmbo kwa Abiola jijini Dar es Salaam na Maiti itasafirishwa kesho Jumaane kwenda Mazimbu Morogo na kutolewa heshima kwa ndugu jamaa na marafiki waishio Morogoro Mjini na Mzumbe.

Jumatano Mwili wa Mpendwa wetu Grace Chao, aliyekuwa Mtumishi wa CRDB Bank Mkoani Mtwara na baade kuhamishiwa Tawi la CRDB Quality Centre jijini Dar es Salaam, utasafirishwa kutoka Mazimbu Morogoro kwenda Marangu Mamba kwa Makundi kwa mazishi.

Mwana Mzumbe na Morogoro kwa Ujumla tunaombwa sana kushirikiana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha Maombolezo.

Taarifa hii ni kwa Mujibu wa Kaka wa Marehemu, Edwin Chao.
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.
Posted by MROKI On Monday, February 18, 2013 2 comments

2 comments:

  1. Oh Grace......hakika Mungu amekupenda zaidi yetu. May ur soul rest in peace.
    We will always miss u, hasa sie ur classmates.
    My condolences to the entire family and all Mzumbe members.

    ReplyDelete
  2. Ni machungu yasiyoelezeka kwetu sote rafiki zako na wanajumuiya wenzako wa Mzumbe.
    Pumzika kwa amani rafiki yangu Grace.
    Daima utakumbukwa sana.

    Pole zangu kwa familia na wanaMzumbe wote.

    Bwana ametoa na ametwaa, jina lake libarikiwe.

    Says,
    Irene Katalyeba.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo