Nafasi Ya Matangazo

January 21, 2013

Nguzi za Zege ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal  umeangukia magari zaidi ya 20 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo bajaji  tatu,yaliyokuwa yamepaki eneo  ambalo hutumika kupaki  wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeelezaa kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa  akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.
Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
Si Magari tu,hata bajaji pia zimeathiriwa vibaya kama uonavyo pichani.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, KinondoniAfande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi
Mmoja wa Maofisa wa Polisi akitazama moja ya gari lililoharibiwa vibaya mara baada ya kuangikwa na ukuta. PICHA ZAIDI BOFYA JIACHIE BLOG
Posted by MROKI On Monday, January 21, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo