Nafasi Ya Matangazo

November 01, 2012



Bendi ya African Stars `Twanga Pepeta’ leo (Ijumaa)  itatambulisha wanamuziki wake wapya mahiri wakati watakapotumbuiza kwenye ukumbi wa Da West Park, Tabata. Wanamuziki watakaotambulishwa ni Kalala Junior aliyerejea kutoka Mapacha Watatu na Mirinda Nyeusi kutoka Mashujaa Band.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho hilo ni maalum kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake. Kapinga alisema kuwa onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.

Kapinga alisema kuwa Kalala pia atatambulisha wimbo wake wa “Nyumbani ni Nyumbani” aliyotunga baada ya kutua Twanga Pepeta mwezi Septemba. “Mirinda Nyeusi pia atatambulisha rapu zake mpya kwenye onyesho hilo ambalo limepangwa kuanza saa moja usiku,” alisema mratibu huyo.

African Stars `Twanga Pepeta” pia inaundwa na waimbaji nguli kama Dogo Rama, Mwinjuma Muumin, Salehe Kupaza, Luiza Mbutu, Msafiri Diof, Amigolas na Badi Bakule. Baadhi ya wapiga vyombo ni Victor Mkambi, Jojo Jummanne, Kizunga, James Kibosho na wengineo.
Posted by MROKI On Thursday, November 01, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo