Nafasi Ya Matangazo

October 03, 2012

 Kiungo Machachari wa Timu ya Yanga,Haroun Niyonzima akijaribu kutaka kumtoka,Shomari Kapombe wa Simba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaoendelea kuchezwa hivi sasa katika uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.Kipindi cha kwanza kimemalizika na Simba wanaongoza kwa bao 1-1 lililofungwa na Mchezaji Amri Kiemba. Yanga wanasawazisha kwa njia ya Penati kupitia kwa Mchgezaji Bahanuzi.

 Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Said Bahanuzi akijaribu kutaka kuwatoka mabeki wa timu ya Simba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara unaoendelea kuchezwa hivi sasa katika uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.Kipindi cha kwanza kimemalizika na Simba wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mchezaji Amri Kiemba.
 Nizar Khalfan wa Yanga akiondoka na mpira.
Beki wa Simba akiondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni mwa timu yake. SOURCE MICHUZI BLOG
Posted by MROKI On Wednesday, October 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo