Nafasi Ya Matangazo

September 05, 2012

Washiriki wa Redds Miss Arusha wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kuwasili katika kambi yao ya mazoezikujiandaa na shindano lao litakalo fanyika Septemba 8, 2012 katika Hoteli ya naura Spring jijini Arusha. Jumla ya waremo 11 wanataraji kucuana vikali kuwania taji hilo.

******
WAREMBO 11 wameingia kambini juzi Jijini Arusha kujifua kwaajili ya shindano la Redd’s Miss Kanda ya Kaskazini 2012, linalotaraji kufanyika jumamosi Septemba 8, 2012 jijini Arusha.


Warembo hao watapanda jukwaani katika Hoteli ya Naura Spring mjini humo kuwania taji hilo linalo shikiliwa na mrembo Stacy Alfred ambaye alinyakua taji la Mrembo mwenye Haiba ya Picha (Miss Photogenic 2011) katika Shindano la Miss Tanzania 2011.

Mwandaaji wa shindano hilo kupitia kampuni ya Jazz Promotions, Emma Mroso amesema kuwa maandalizi yote ya shindano hilo yanakwenda vyema na warembo wapo katika afya njema.

Aidha Mroso amewataja warembo walioingia kambini na wanaendelea na mazoezi yao kuwa ni Mishi Mziray, Dalina Hashim, Anita Mboya, Highmanna Lyimo, Anande Radhiel, Waridi Frenk, Buya Ernest, Lucy Stephano, Neyla Hashim, Trovina Mpanda na Theresia Kimolo.

Mratibu huyo amesema kuwa warembo hao walistaili kuwa 12 ikiwa ni warembo 3 kila mkoa kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga ispokuwa mshiriki mmoja Sara Benjamin anaumwa na yupo Nairobi kwa matibabu.

Shindano hilo linataraji kupambwa na burudani kali kutoka kwa Banan Zoro na kundi zima la B Band pamoja na wasanii wengine mbalimbali wa jijini Arusha.

Shindano la Redd’s Miss Kanda ya kaskazini 2012 limedhaminiwa na  Redd’s Original,  Dodoma Wine, Naura Springs Hotel,  Brazil Lounge,  Father kidevu Blog,  Modern holdings EA ltd, Honeys furniture, Little Roses, Jazz collection, Camro Insurance Services,   Eannaso,  Anyor Designs,   Triple A FM, Ndeku hair salon, Compumania celltronics,TLK investments, Computer and Secretarial College,  Arusha Art,  Cyber Net, Riverside Shuttle, eo security na Authentic Emergency Services.
Posted by MROKI On Wednesday, September 05, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo