Nafasi Ya Matangazo

September 03, 2012

Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kliniki hiyo ambayo ilikuwa inafanyika Nairobi, Kenya.
**********


Kliniki ya Airtel Rising Stars imefikia mwisho, Nairobi -  Kenya. Kliniki hiyo ambayo ilizinduliwa Jumatatu ya tarehe 27 Agosti ilihudhuriwa na vijana zaidi ya 50 kutoka barani Afrika. 
 
Washiriki wa kliniki hiyo wametumia muda wa wiki moja kupata mafunzo kutoka kwa waalimu wa soka ya vijana kutoka Klabu ya Manchester United.
 
Vijana walihudhuria kliniki hiyo walichanguliwa kutokana na kufanya vyema kwenye michuano ya Airtel Rising Stars Pan-Afrika, michuano yenye lengo la kutafuta na kukuza vipaji vya soka.

Mpango wa Airtel Rising Stars – ambao umeingia mwaka wa pili – imetajwa kuwa moja ya michuano mikubwa barani Afrika, huku timu 18,000, wachezaji 324,000 kutoka nchi 15 za Afrika zikishiriki kwa mwaka huu. Pia, imekuwa ni michuano ya kipekee kwa kushirikisha wasichana.

Akiongelea kuhusu kliniki hiyo, Ofisa Masoko Mkuu wa Airtel Afrika, Andre Beyers anasema, ‘Kwa mara nyingine mafanikio ya kliniki ya mwaka huu imeonyesha jinsi soka inaweza kuunganisha jamii na makabila yote pamoja. Na kuongeza michuano ya Pan-Afrika ambayo imeleta vijana kutoka maeneo mbali mbali barani Afrika, kuzoena na kubadilishana maadili ya kila mmoja, kwa hakika ni hatua moja kubwa kwa maisha ya kila mmoja’.

Kwenye sherehe za ufungaji wa kliniki hiyo, kila mshiriki alipokea medali ya ushiriki ambayo ilitolewa kulingana na hadhi ya Klabu ya Manchester United. Wakati wa kliniki hiyo, vijana wameweza kujifunza mambo mbali mbali kama – ukabaji, kufunga, kuzuia na hata mbinu zingine za kijanja za soka – na kushauriwa kuzitumia kila wanapokuwa uwanjani.

Klikini hiyo ni mpango wa miaka mine wa ushirikiano baina ya Manchester United na Airtel Afrika kwa shule za soka za vijana ya Manchester United kutoa mafunzo kwa vijana chipukizi. Shule za soka za vijana za Manchester United zimekuwepo kwa miaka 12 sasa na utoa mafunzo kama haya kwa wanafunzi zaidi ya 120,000 duniani kila mwaka.
Posted by MROKI On Monday, September 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo