Nafasi Ya Matangazo

September 10, 2012

Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa TangaAmina Mwidau (CUF), akikabidhi zawadi ya kikombe cha ushindi kwa Nahodha watimu ya Chuda FC Ibrahimu Bodwe, baada ya timu yake kuibuka kidedea katikamichuano ya Haniu Cup, katikati ni Mratibu wa Mashindano hayo Mohammed Haniu.
**********
Na Father Kidevu Blog, Tanga
HATIMAYE timu ya Chuda FC ya Chumbageni Jijini Tanga, imetwaa ubingwa wa mashindano ya Haniu Cup, kwa kuichapa kwa mikwaju ya penati timu ya Jiwe FC yenye maskani yake Tanga Sisi.

Fainali hizo ambazo zilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga, zilikuwa za aina yake ambapo hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa timu hizo ziliweza kutoka sare ya bao 1-1.

Chuda, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4 kwa 1 hali iliyowafanya mashabiki wa timu hiyo kutoka na shangwe uwanjani.

Akizungumza katika mashindano hayo kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), alisema ni muhimu kwa mkoa huo kuwa na kiwanja mbacho kitakuwa ni mahususi kwa ajili ya kuibua vipaji wa soka mkoani humo.

“Mimi kama Mbunge wetu wa Viti maalum na diwani wenu nina wajibu wa kusimamia kwa karibu shughuliza maendeleo ikiwemo kunua soka katika mkoa wetu huu wa Tanga.

Mkoa huu ni chimbuko la michezo nchini na katika hili nitahakikisha ninawasilisha hoja katika kikao cha Jiji ili kuweza kijengwe kiwanja maalum ambacho itakuwa Soka Academy.
Posted by MROKI On Monday, September 10, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo