Nafasi Ya Matangazo

September 10, 2012

Diwani wa Kata ya Dodoma mjoni, David Madole akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya Atlantic mara baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya Safari Pool ngazi ya mkoa, Mkoa wa Dodoma yaliyo malizika mjini hapo mwishoni mwa wiki.


 *****     *****
Na Father Kidevu Blog, Dodoma
TIMU ya mchezo wa pool ya Atlantic yenye makazi yake Majengo Mjini Dodoma, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya pool ya 'Safari Lager National Pool Championships 2012' baada ya kuibamiza klabu ya Florida yenye makazi yake Barabara ya Bahi, 13-8 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ngazi ya mkoa yaliyofanyika katika Klabu ya Atlantic mjini Dodoma

Atlantic ilitwaa ubingwa huo na kujinyakulia fedha taslimu Sh.700,000 na Kikombea mbapo pia kuwa wawakilishi wa mkoa huo katika fainali za Kitaifa zitakazofanyika Septemba 26 mwaka huu mkoani Mwanza kwa kushirikisha vilabu 16 ambavyo vitakuwa mabingwa kwenye mikoa yao.

Florida ilikamata nafasi ya pili na kuzawa kitita cha shilingi 350,000  na mshindi wa tatu katika mashindano hayo  ni Klabu ya Tiger yenye makazi yake eria C, ambao walizawadiwa shilingi 200,000 na wanne ni klabu ya  Car Wash ya Bara bara ya Bahi ambao walizawadiwa shilingi 100,000.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanaume), Abdu Forty kutoka klabu ya Florida alitwaa ubingwa kwa kumchapa Athuman Gora wa klabu ya White Horse 4-0, na kujinyakulia kitita cha shilingi 350,000 ambapo Abdu Forty alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 200,000, wakati Mohamed Jafari wa Klabu ya Atlantic alikamata nafasi ya tatu na kuzawadiwa shilingi 150,000.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanawake),Monica Simule alitwaa Ubingwa na kuzawadiwa Shilingi 250,000/= na nafasi ya pili ni Happy Mkumbo.

Zawadi kwa washindi wote zilikabidhiwa na Diwani wa Dodoma Mjini, David Madole ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo katika Mkoa Dodoma.
Posted by MROKI On Monday, September 10, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo