Nafasi Ya Matangazo

August 22, 2012

Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa watangazaji wa redio hiyo Lovenes Love na Adam Mchomvu wakati walipokuwa wakiongea na wasikilizaji wa redio ndani ya Tanga katika amsha amsha ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalotegemea kufanyika tarehe 26.8.2012 Uwanja wa Mkwakwani. Tamasha hilo litakalopambwa na msanii maarufu wa kimataifa kutoka nchini Kenya Prezzoo.
Mtangazaji wa Clouds Fm Adam Mchomvu akionesha t-shirt ambazo zimetoka kwa ajili ya kusherekea tamasha hilo la Fiesta 2012.
Mwanadada Loveness Love akisababisha ndani ya amsha amsha ya tamasha la Fiesta linalofanyika wikend hii ndani ya Tanga.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga akiendeleza harakati za kukamata matukio ndani ya kitaa cha Chumbageni, pale Clouds Fm ilipotembelea vijana hao wa maskani na kupata mawili matatu kuhusiana na tamasha hilo.
Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
...vijana wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga, pembeni yake ni Adamu Mchomvu.
Posted by MROKI On Wednesday, August 22, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo