Nafasi Ya Matangazo

June 13, 2012

 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw Rene Meza akielezea jinsi Vodacom ilivyochangia zaidi ya shilingi bilioni 700 katika malipo ya kodi ya serikali alipokutana na  waandishi wa habari mjini Dodoma.
 Mhariri wa gazeti la The Citizen, Peter Nyanje akiuliza swali. Pamoja nae  katikati ni mhariri wa gazeti la Daily News  John Kulekana na kushoto ni mhariri wa gazeti la Habari Leo  Mgaya Kingoba.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani)
Mwandishi wa gazeti la The Guardian Bw. Florian Kaijage akiuliza swali kuhusiana na Vodacom Tanzania kuchangia zaidi ya shilingi bilioni 700 katika kodi za serikali katika mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza(Hayupo Pichani), kushoto kwake ni mhariri wa gazeti la Mwananchi Bw. Neville Meena.
 Wahariri mbali mbali wa vyombo vya habari wakinukuu maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza (hayupo pichani), akielezea jinsi Vodacom ilivyochangia zaidi ya shilingi bilioni 700 katika malipo ya kodi ya serikali alipokutana na  waandishi wa habari mjini Dodoma.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiwaelezea uchangiaji wa Vodacom wa zaidi ya Shilingi bilioni 700 katika kodi za serikali alipokutana nao mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza akishauriana jambo na Afisa Mkuu wa Mahusiano Bi Mwamvita Makamba na Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Tiaan Botha (kulia)
 Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Tiaan Botha akishauriana jambo na Afisa Mkuu wa Sheria Bw. Walarick Nittu (wa pilli kulia), Afisa Mkuu wa Mtandao  Bw. Alec Mulonga (kulia) na mkuu wa kitengo cha Uhandisi wa Vodacom Tanzania Bw. George Magonyozi (kushoto)
Posted by MROKI On Wednesday, June 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo