Nafasi Ya Matangazo

June 26, 2012

MASHINDANO ya kumsaka mrembo wa Miss  Universe Tanzania 2012  yatafanyika Ijumaa hii kwenye ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa  yaliyopo Posta  jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Comm  unications, Maria Sarungi Tsehai amesema leo kuwa mashindano hayo yatawashirikisha jumla ya warembo 20 kutoka katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.

Mikoa hiyo ni Manyara, Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Kilimanjaro na wenyeji Dar es Salaam na kuongeza warembo wote wanaendelea na mazoezi chini ya wakufunzi walioboea katika masuala ya urembo. “Tunatarajia kuwa na mashindcano bora ili kuweza kumapata mrembo ambaye atatupa sifa katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa  kwa Flaviana Matata mwaka 2007 ambapo alishika nafasi ya saba katika mashindano yaliyofanyika nchini Mexico,” alisema Maria.

Maria aliwataja warembo hao  kuwa ni Bahati Chando, Aisha Maulidi, Catherine Mpulule, Cecilia Moses, Consolata Mosha, Devotha Keregese, Doris Mollel, Doreen Mapunda na Edith Tesha. Wengine ni Getrude Asanterabi, Jescha Tiba, Kundi Mligwa, Lilian Kolimba, Mary Joel, Naomi Joseph, Nyaso Malilo, Neema Mpanda, Susan Manoko, Theodora Msenya na Winfrida Dominic.

Alisema kuwa shindano hilo limedhaminiwa na gazeti  la The Citizen, gazeti dada la Mwananchi kwa kushirikiana na wadhamini wengine,  Le Grand Casino, Urban Rose Hotel, Amina Design, Dodoma Hotel na New York  Film Academy.

Maria alisema kuwa shindano hilo litaanza saa 1.00  usiku kwa warembo hao kupita jukwaani wakiwa katika aina mbalimbali za mavazi kama vile ya ubunifu na lile la usiku. Alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo kubwa la urembo yamekamilika na kinachosubiliwa ni siku ya shindano hili kupata mrithi wa Miss Universe anayemaliza muda wake Nelly Kamwelu.

Alifafanua kuwa wameboresha mashindano ya mwaka huu  na wanatarajia kuwa na mashindano bora kabisa tofauti  na  ya  miaka ya nyuma.

Posted by MROKI On Tuesday, June 26, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo