Nafasi Ya Matangazo

June 28, 2012

 Meneja huduma za jamii bi Hawa Bayumi  akijitolea damu katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na kuhusisha wafanyakazi wa Airtel kuchangia damu kwa mfuko wa taifa wa kuhifadhi damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu. Zoezi hilo la kuchangia damu limefanyika leo siku nzima katika makao makuu Moroco. 
 Bi Helena  Mteti Meneja Muhakiki wa Kodi Airtel akipata ushauri kutoka kwa muugizi Bi Elizabeth Mgaya kutoka kitengo cha damu salama cha taifa kabla ya kuanza zoezi la kuchangi damu lililoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel likishirikisha wafanyakazi wake  Zoezi hilo la kuchangia damu limefanyika leo siku nzima katika makao makuu Moroco.
Mfanyakazi wa Airtel Bwana Greyson Mapunda akijitolea damu katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na kuhusisha wafanyakazi wa Airtel kuchangia damu kwa mfuko wa taifa wa kuhifadhi damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu. Zoezi hilo la kuchangia damu limefanyika leo siku nzima katika makao makuu Moroco. akitoa huduma ni Bwana James Semba kutoka Kitengo cha damu salama cha taifa.
*********
Alhamisi, Juni 28 2012, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeandaazoezi la kuchangia damu litakalohusisha wafanyakazi wake kuchangiadamu kwa lengo la kuokoa maisha ya  wagonjwa wanaohitaji damu, hii nimoja  kati ya shughuli za Airtel katika kusaidia jamii

Akiongea wakati wa zoezi la kutoa damu lililofanyika katika makao makuu ya Airtel Mkurugenzi Rasilimali watu Perece Kirigiti alisema”Airtel inandeleza dhamira yake ya kusaidia na  kuchangia katikashughuli za kijamii na leo tunashirikisha wafanyakazi wetu kuchangiadamu katika kukiwezesha kitengo cha  damu salama cha taifa kuwa nahifadhi ya damu ya kutosha kukidhi mahitaji ya wagonjwa na kuwezakuokoa maisha ya wagonjwa.

Tutakuwa na zoezi hili siku nzima ya Alhamisi hapa Ofisini makao makuu Dar es salaam ambapo madaktari kutoka kitengo cha taifa cha kutoa damu wataendesha zoezi la kutoa damu kwa wafanyakazi na wageni watakaojitolea kuchangia. Wafanyakazi wetu wanayofuraha kuona wanaokoa maisha ya watanzania nchini na kwa jinsi hiyo tunatimiza majukumu yetu katika kusaidia jamii inayotunzunguka.

Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamiii bi Hawa Bayumi akichangia kuhusu jitihada hizi alisema” hii ni moja kati ya jitihada zetu za kuwawezesha wafanyakazi wetu na wadau mbalimbali kuona jukumu lao katika kusaidia jamii, na kwa mwaka huu wito ni  changia damu ili kuokoa maisha”

Zoezi zima la utoaji damu litahusisha kujaza fomu,  mahojiano na uchunguzi wa afya utakaofanywa kwa kufata kanuni za tiba, kisha kufatiwa na utoaji damu utakaochukua takribani dakika 10 ambapo mililita 450 za damu zinategeme kuokoa maisha ya mtu mmoja Tanzania inahitaji kiasi cha damu cha unit 350,000 kwa mwaka kwa ajili ya huduma za dharura za tiba ambapo kwa sasa kitengo cha  damu salama cha taifa kinakusanya unit 115,000- 120,000 kwa mwaka hivyo kuwa na mapungufu ya kiasi cha unit 235,000.

kitengo cha  taifa cha kutoa  damukitengo cha  damu salama cha taifa wa damu kwa mwaka huu wa 2012 na kufanya juhudi za kukusanya unit 180,000, hivyo inatoa wito kwa watanzania wenye afya walio na umri kati ya  18 na 65 na uzito wa 50kgs kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu.
Posted by MROKI On Thursday, June 28, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo