Nafasi Ya Matangazo

May 16, 2012

Timu ya Majaji kutoka kushoto ni Proffesor Jay, Henry Mdimu, Queen Darleen na Juma Nature
Dodoma Winners:
Halima Ramadhani, Juma Madaraka na Issa Dubat
Mwanza Winners
Bertha Dennis, Chrostian joachim na Marcus Antony
Moshi Winners
Gaspar Fadhil Sungura, a.k.a Chagga Boy, Charlz Mushi na Atufigwege Mwailunga.
Mbeya Winners
Neema Aggrey, Furaha Challi na Amina Chibaba



Na Mwandishi Wetu
Washindi wa msako wavipaji unaodhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, wiki hii umefikia hatua ya nne ambapo umefanikisha kupata washindi 12 ambao wamepata nafasi ya kurekodi nyimbo zao tayari kwa kuanza safari yao ya kisanii kupitia muziki.

Kwa mujibu wa waratibu wa zoezi hilo kampuni ya Frontline Novelli, tayari usaili umeshapita katika jumla ya mikoa minne na kila mkoa walikuwa wakichukuliwa washindi watatu watatu.

Akiifafanua zaidi kuhusiana na mchakato huo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Frontline, Irene Kiwia alisema washindi hawa watatu wa kila mkoa mara wanapopatikana hupewa nafasi ya kurekodi wimbo, kila mmoja na kisha kufanya wimbo wa pamoja wakishirikiana wote watatu.

Baada ya kurekodi washindi hawa watatu wote wanashiriki katika tamasha la washindi la mkoa huo ambapo kati yao mmoja atakayefanya vema jukwaani ndio anapata nafasi ya kushiriki tamasha kubwa la washindi litakalofanyi9ka mapema mwisho wa mwezi huu jijini dar es salaam.

Mikoa ambayo imeshatembelewa mpaka sasa ni Dodoma, Mwanza, Moshi na Mbeya ambapo washindi wake tayari wamesharekodi na katika mikoa ya Dodoma, Moshi na Mwanza, washiriki wa tamasha kubwa kabisa litakalofanyika mkoani Dar es salaam wameshapatikana.

Kutoka Dodoma ambako ziara ya kusaka vipaji hivi ilianzia Halima Ramadhani, Juma Madaraka na Issa Dubat waliibuka washindi ambapo baada ya Tamasha kufanyika, Issa Dubat ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara CBE aliwafunika wenzake na ndiye aliyefanikiwa kuwakilisha wenzake katika Tamasha kubwa la washindi jijini Dar es Salaam.

Jijini Mwanza, walipatikana Bertha Dennis, Chrostian joachim na Marcus Antony
Safari haikuishia hapo ikaingia mkoani Kilimanjaro, huku zoezi makini likisimamiwa na majaji mahiri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, jambo ambalo Kilimanjaro Premium Lager imeonekana kutumia busara kubwa kuwapata.
Jaji wa kwanza ni mhariri wa Burudani wa gazeti la mwananchi, ambaye kabla ya hapo amekuwa mwandishi wa habari za burudani tangu mwaka 1998, na kushiriki matamasha na kuratibu shughuli mbali mbali za burudani likiwemo shindano la Mfalme wa Rhymes ambalo lilimuibua Afande sele kutoka Morogoro.
Jaji wa Pili na Joseph Haule, a.k.a Profesa Jay ambaye ni mwanamuziki mwenye tunzo nyingi kuliko wanamuziki wote wa kiume nchini, ambaye amekuwa katika tasnia hii takriban miaka kumi na moja sasa huku akionekana kutoshuka kimuziki kutokana na ubunifu wake.
Jaji wa tatu ni Juma Kassim Nature, mwanamuzki pia wa muziki wa kizazi kipya aliyekuwepo kwa miaka mingi kutoka katika kundi la TMK Wanaume Halisi na Jaji wa nne ni Queen Darleen, mshindi wa mwaka huu wa tunzo ya mwanamuziki bora wa Ragga.
Huko Kilimanjaro kwa mara ya kwanza akapatikana mwanamuziki bora wa Hip Hop kutoka mkoani ambaye ndiye atakayeiwakilisha Moshi katika tamasha kubwa la washindi. Jamaa anaitwa Gaspar Fadhil Sungura, a.k.a Chagga Boy ambaye kwa pamoja alishiriki tatu bora ya Moshi akiwa na Charlz Mushi na Atufigwege Mwailunga.

Kazi nyinmgine kubwa nzuri imefanywa na Majaji wiki hii ambapo Mbeya nayo imepata washindi wake katika shughuli iliyofanyika Club Vibes, na mpaka mwisho wa siku, Neema Aggrey, Furaha Challi na Amina Chibaba, hawa watajumuika na washindi wab tunzo za Kili katika Tamasha litakalofanyika katika uwanja wa Sokoine ambapo mwisho wa siku mmojawapo atapata nafasi ya kushiriki katika tamasha kubwa zuri la washindi ambalo litakuwa likifunga dimba la matamasha ya washindi ya tunzo za Kili za mwaka huu.

Wakiongea kwa nyakati tofauti Majaji wa shindano hilo ambalo huwa gumzo kila linapotua kwenye mkoa husika waliisifu kwanza kampuni ya Bia ya TBL kwa kuonesha nia nzuri ya kutafuta vipaji na kuviendeleza.

kwa upande wake Juma Nature alisema huu ni wasaa mzuri kwa wanamuziki chipukizi kuonesha uwezo wao kwani wakati wa enzi zake yeye, hapakuwa na nafasi kama hizi, walitumia nguvu sana kujulikana tofauti na wanamuziki wa sasa ambao wameanza muziki kukiwa na vyombo vingi vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ambayo inasaidia sana kutambulisha kazi za wasanii.

Akiongelea hili Mkurugenzi wa Frontline Bi Kiwia amesema lengo kuu ni kutafuta vipaji vilivyojificha ambavyo vinapatikana kwa wingi mikoani na huko si rahisi kuviona na ndio maana Kilimanjaro kama bia ikaamua kuvifuata huko viliko na kuvivumbua na kuvipa nafasi ya kuonekana kwa jamii ya watanzania na kuamua kuhusiana na vipaji hivi.

"Tatizo ni kwamba watu wanaamini kila kitu kiko Dar jambo ambalo inabidi uliangalie kwa umakini kabla hujalisema. Ukweli mikoani kuna vitu ila tatizo ni tutavionaje?".

Usaili wa mwisho utafanyika mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki hii ambapo napo wasanii watatu watapatikana na kati yao, mmoja tu ndio atashiriki tamasha kubwa la jijini Dar
Posted by MROKI On Wednesday, May 16, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo