Nafasi Ya Matangazo

May 23, 2012

Mwenyekiti wa (PAC) John Cheyo (Mwenye koti),Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile(mwenye Kaunda ya blue) pamoja na Wajumbe ya Kamati ya (PAC) na baadhi ya Uongozi wa watendaji wa serikali Mkoani DSM wakikgua baadhi ya makazi ya waathirika wa mabomu ya Mbagala Mkuu jana.
Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustini Ndugulile (kulia) akizungumza na baadhi ya waathirika ya mabomu ya Mbagala Kuu baada ya kumaliza kikao ambacho waathirika hao walikutana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na kutoa malalamiko mbalimbali ikiwemo madai ya kupunjwa malipo ya fidia, Mabomu ya Mabagala Kuu yalitokea mwaka 2009 Mkoani Dar es Salaam na kusababisha maafa ya makazi na vifo.
Mwenyekiti wa (PAC) John Cheyo akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Peniel Lyimo
Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile (mwenye Kaunda ) akiwasikiliza baadhi ya waathirika wa mabomu ambao wamechukua hundi yao ya malipo na kuwawezesha kukarabati makazi yao . Mbunge Ndugulile aliongozana na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Mwenyekiti wake John Cheyo hayupo Pichani
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) John Cheyo (Mwenyekoti) na Katibu wa Kamati ya (PAC) Ramadhan Issa Abdallah (kushoto) pamoja na baadhi ya wanakamati na watendaji wa Mkoa wa DSM wakiangalia orodha yenye majina ya malipo kwa waatihirika wa mabomu ya Mbagala Kuu walipotembelea huko Mbagala Kuu na kuangalia maeneo ya wakazi hao ambayo mengine yamekarabatiwa. Mwenyekiti huyo amewashauri baadhi ya waathirika hao kwenda kuchukua hundi zao haraka kabla ya zoezi la malipo kufungwa
Muathirika wa mabomu ya Mbagala yaliyotokea mwaka 2009 mkoani Dar es Salaam Mzee Steven Gimongi  (kushoto) akitoa maelezo jinsi alivyoathirika mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) John Cheyo (mwenye koti katikati) pamoja na ujumbe wake walipotembelea Mbagala Kuu na kuungalia sehemu hiyo pamoja na kuzungumza na waathirika ambao amewashauri wale ambao hawajakwenda kuchua hundi za malipo yao, waende haraka wakazichukue kabla zoezi hilo kufungwa.
Baadhi ya Waathirika wa mabomu ya Mbagala wakiwa katika mkutano na Kamati ya PAC. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Posted by MROKI On Wednesday, May 23, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo