Nafasi Ya Matangazo

February 16, 2012

Kikosi cha timu ya soka ya Simba kinacho shiriki Ligi kuu ya soka Tanzania Bara maarufu kama ligi ya Vodacom, kimekuwa bora zaidi baada ya kutoa wachezaji tisa wanaounda kikosi cha timu ya taifa kitakacho vaana na Msumbiji.

Kikosi cha Azam FC nacho kutoka ligu kuu, kimeweza kuwa cha pili baada ya kutoa wachezaji 6 huku watani na mahasimu wakubwa wa Wekundu wa Msimbazi Simba wakiambulia wachezaji watatu pekee katika kikosi hicho.

Kwa mujibu wa majina yaliyotangazwa hii leo na Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Jan Poulsen leo (Februari 16 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Paulsen alitaja majina kutoka simba kuwa ni Juma Kaseja, Masoud Cholo,Uhuru Selemani, Kelvin Yondani ,Jonas Gerard , Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyoso na  Juma Jabu.

Wachezaji waliotolewa kutoka kikosi cha matajiri wa Ilala, Azam FC ni Mwadini Ali, Aggrey Morris, Salum Abubakar , Abdi Kassim, John Bocco na Mrisho Ngasa.

Timu ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi na Jumamosi hii inashuka dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kumenyanna na warabu Zamaleki imemtoa Shabani Kado, Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika.

Timu zingine zilizotoa wachezaji hao wanaunda kikosi cha timu ya taifa ni pamoja na Mtibwa Suger iliyo na wachezaji wawili Hussein Javu na Shabani Nditi  huku Nsa Job akitoka Villa Squad na wachezaji wa kulipwa ni  Nizar Khalfan (Philadelphia Union, Marekani) na  Ally Badru Ally (Canal Suez, Misri).

Kabla ya kuivaa Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi itakayochezwa Februari 29 mwaka huu, kikosi hicho kinatarajia kucheza mechi ya kirafiki Februari 23 mwaka huu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) itakayofanyika kwenye uwanja huo huo.

Wachezaji wapya walioitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho kitakachoingia kambini Februari 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni viungo Jonas Gerald (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Posted by MROKI On Thursday, February 16, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo