Nafasi Ya Matangazo

December 20, 2011

BENDERA AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA WARATIBU WA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kushoto), akiagwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emmanuel Humba baada ya kufungua kongamano la kwanza la Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, mjini Morogoro jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa CHF, Athuman Rehani.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa CHF, Athuman Rehani akitoa mada kuhusu mkakati wa CHF kwa wote.
Baadhi ya Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, wakishiriki katika kongamano la kwanza la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za mfuko huo, lililofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, mjini Morogoro jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa CHF, Athuman Rehani wakati wa kongamano hilo.
Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Khamis Mdee akifafanunua mambo wakati wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (kulia), akiwaeleza waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), umuhimu wa kuuboresha mfuko huo kwa faida kizazi cha sasa na kijacho, wakati wa kongamano la kwanza la waratibu wa mfuko huo nchini, lililofanyika kwenye Hoteli ya Kisasa ya Nashera, mjini Morogoro.
Moja ya makundi ya Waratibu wa CHF, wakijadiliana jinsi ya kuweka mikakati ya uboreshaji wa mfuko huo.
Posted by MROKI On Tuesday, December 20, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo