Nafasi Ya Matangazo

September 03, 2011

Mgeni rasmi katika shindano la kumtafuta Miss Talent wa Vodacom Miss Tanzania 2011, Mwanamitindo wa kimataifa Cynthia Kanema ambaye pia aliwahi kuwa Miss Zambia 2003 akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo na kupokelewa na wenyeji wake Suleiman Masoud Nassor  (katikati) na Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye. Shindano la Miss Talent litafanyika leo katika Hotel ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach Dar es Salaam.
Mwanamitindo wa kimataifa Cynthia Kanema ambaye pia aliwahi kuwa Miss Zambia 2003 akizungumza na waandishi wa habari.
Mgeni rasmi katika shindano la kumtafuta Miss Talent wa Vodacom Miss Tanzania 2011, Mwanamitindo wa kimataifa Cynthia Kanema ambaye pia aliwahi kuwa Miss Zambia 2003 akiwaameongozana na Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo.  Shindano la Miss Talent litafanyika leo katika Hotel ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Saturday, September 03, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo