Nafasi Ya Matangazo

September 21, 2009

Mbunge wa Ilala, Mheshimiwa Mussa Hassan Zungu (kulia) akisalimiana na mlezi wa Madrasatil Neema Maumba, Hijat Neema Maumba (kushoto) jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kupata chakula maalum kilichoandaliwa jana na Kampuni ya Zain Tanzania kwa watoto wa Madrasahiyo iliyopo Buguruni ikiwa ni sehemu ya kufurahia Siku Kuu ya Eid El-Fitr kwa Madrasat hiyo ambayo inalea watoto yatima na walio katika mazingira magumu. Wengine katikati kutoka kushoto ni wafanyakazi wa Zain Tanzania, Celine Njuju, Beatrice Singano Mallya na Ismail Katumba.
Jasmin Kayaga (kushoto) na Yusra Omar (katikati) wa Madrasat Neema Maumba ya Buguruni jijini Dar es Salaam wakila chakula jana pamoja na Meneja Mawasiliano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya (kulia) ikiwa ni sehemu ya kuazimisha Sikuu ya Eid Fitr. Zain iliandaa chakula maalum kwa madrasa hiyo ambayo inalea watoto yatima na walio katika mazingira magumu.
Baadhi ya watoto wa Madrasat Neema Maumba ya Buguruni jijini Dar es Salaam wakila chakula jana ikiwa ni sehemu ya kuazimisha Sikuu ya Eid Fitr. Zain iliandaa chakula maalum kwa madrasa hiyo ambayo inalea watoto yatima na walio katika mazingira magumu.
Posted by MROKI On Monday, September 21, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo