Nafasi Ya Matangazo

March 27, 2009

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema (Pichani) amefanya mabadiliko madogo ndani ya uongozi wa Jeshi hilo kwa kumteua Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas kuwa Kamanda mpya wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kaimu Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Juma Said Ally alisema kuwa, kabla ya uteuzi huo Kamanda Sabas alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ambapo sasa anakwenda Temeke kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Emmanuel Kandihabi anayehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo.

Aidha Kaimu Msemaji huyo aliongeza kuwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi pia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi George Mayunga kuwa Kamanda mpya Mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya marehemu Kamishna Msaidizi Adhihaki Rashid aliyefariki hivi karibuni.


Maafisa wengine waliohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mnadhimu Mkuu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Robert Boaz aliyekwenda kuwa Kamanda wa Mkoa wa Mtwara kufuatia kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Mkoa huo marehemu Kamishna Msaidizi Ephrahim Mrema.

Naye Kamishna Msaidizi Sifuel Shirima ameteuliwa kuwa Kamanda mpya wa Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Jamila Msafiri aliyestaafu. Awali ACP Shirima alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Mkoa huo wa Lindi.

SSP Jacob Maruanda anatoka OCD Dodoma kwenda Ofisi ya RPC Mkoa wa Rukwa, SSP Simon Haule anatoka OCD Viwanja vya Ndege Dsm kwenda kuwa OCD Wilaya ya Dodoma, SP Justine Kiita kutoka OCD Wilaya Igunga na kuwa Mnadhimu Msaidizi Viwanja vya Ndega Dsm na SP Justine Shoo kutoka Ofisi ya RPC Shinyanga na kwenda kuwa OCD Wilaya ya Igunga.

Wengine ni SP Charles Chalya kutoka OC CID Wilaya ya Lindi kuwa OCD Viwanja vya Ndege Dsm, SP Camilius Wambura kutoka OC CID Buguruni Dsm kwenda kuwa RCO Kinondoni, SP Koka Moite kutoka OCS Kituo cha Polisi Magomeni kuwa OC CID Ruangwa Lindi na ASP Buluba Balekele kutoka Afya Kuu kwenda kuwa OCS Kituo cha Polisi Ruangwa Lindi.

Kamishna Msaidizi Juma alisema kuwa uhamisho huo ni wa kawaida ndani ya Jeshi la Polisi unaoenda sanjari na kuziba nafasi zilizoachwa wazi na maafisa waliofariki pamoja na wale wanaostaafu kwa mujibu wa sheria ambapo pia amesema IJP ameagiza utekelezwe mara moja.
Posted by MROKI On Friday, March 27, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo