Serikali imewataka wanahabari kutumia kalamu zao na weledi wao kuongeza uelewa wa umma kuhusu Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, 2025, kwa kuzingatia takwimu sahihi, kueleza fursa zinazotokana na Sera hiyo, pamoja na namna inavyolenga kuimarisha matumizi bora ya rasilimali za umma.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) wakati akifungua mafunzo ya Siku mbili ya Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wamiliki wa Mitandao ya kijamii ya Habari, katika ukumbi wa Hoteli ya Timeless mjini Morogoro.
Mheshimiwa Munde amesema kuwa, vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kujenga uelewa wa wananchi kuhusu sera na namna inavyogusa matumizi ya rasilimali za umma, pamoja na namna mnyororo wa ugavi unavyohusisha hatua mbalimbali, ikiwemo utambuzi na upangaji wa mahitaji, ununuzi, ugomboaji, upokeaji, utunzaji na uhifadhi, matumizi, usambazaji pamoja na uondoshaji wa bidhaa, vifaa na mali.
“Usimamizi wa mnyororo wa ugavi una athari ya moja kwa moja katika namna rasilimali za umma zinavyotumika na namna huduma zinavyowafikia wananchi, hivyo Sera hii ni nyenzo muhimu katika kuimarisha ufanisi, uwajibikaji, uwazi na matumizi yenye tija ya fedha za umma katika shughuli za mnyororo wa ugavi katika Sekta ya Umma,"amesema Mheshimiwa Munde.
Amesema kuwa, utekelezaji wa sera hiyo unatoa fursa ya kuimarisha ushiriki wa wazalishaji, kampuni na watoa huduma wa ndani katika shughuli za mnyororo wa ugavi, na hatua hizo zinaangalia pia kuongeza matumizi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, kuendeleza wataalamu wa ndani na kutumia teknolojia katika shughuli mbalimbali za mnyororo wa ugavi.
“Wahariri na Waandishi wa Habari ni kiungo muhimu kati ya Serikali, wadau na wananchi katika kufikisha taarifa hizi za kisera na kitaalamu kwa lugha rahisi na inayoeleweka ndio maana mpo hapa leo kupata uelewa zaidi kuhusu Sera hii,”amesema Mheshimiwa Munde.
Ameongeza kuwa,jukumu la vyombo vya habari halipaswi kuishia katika kuripoti shughuli za utekelezaji wa sera, bali pia kufuatilia maendeleo, kubaini changamoto na kuibua maeneo yanayohitaji.









No comments:
Post a Comment