August 23, 2026

AZAM MARINE YAONGEZA NGUVU KUSAFIRISHA MASHABIKI AFCON 2027

Kampuni ya Azam Marine imeanza maandalizi ya kuimarisha huduma za usafiri wa majini kuelekea michuano ya AFCON 2027, ikiwamo kuongeza meli mpya ya Kilimanjaro 9 iliyowasili Januari mwaka huu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Marine, Bw. Abubakari Aziz Salim, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza uwezo wa kusafirisha mashabiki, wachezaji na viongozi kati ya Dar es Salaam na Zanzibar wakati wa michuano hiyo.

Bw. Salim amesema kampuni hiyo ina uwezo wa kusafirisha hadi abiria 15,000 kwa siku, huku ikijivunia uzoefu wa miaka 33 katika sekta ya usafiri wa majini.

Aidha, amesema Azam Marine itatoa ajira za muda mfupi ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya wasafiri wakati wa AFCON 2027.

Amewataka Watanzania kutumia fursa hiyo kuitangaza Tanzania kwa ukarimu na huduma bora, akisisitiza kuwa urithi wa michuano hiyo utategemea namna nchi itakavyojiandaa na kutumia fursa zitakazojitokeza.

“Tutumie platform hii ya AFCON 2027 kuiweka Tanzania katika mioyo ya wageni,” amesisitiza Bw. Salim.

No comments:

Post a Comment