Familia ya ASAS imetangaza Kwa masikitiko makubwa kifo cha Al Haj Mzee Jaffer Abri (ASAS), ambaye amefariki leo asubuhi mjini Istanbul, Uturuki.
Kwa mujibu wa taarifa ya Familia hiyo, Swala ya Janaza pamoja na mazishi yamefanyika mjini Istanbul baada ya Swala ya Alasiri, kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (SWT) amsamehe madhambi yake, amrehemu kwa rehema Zake zisizo na mipaka, amjaalie Pepo ya Jannatul Firdaus, na awape subira, faraja na nguvu familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu mzito.
No comments:
Post a Comment