Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akifanya mazungumzo na
watendaji wa Benki ya NMB kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuweka
mikakati ya pamoja ya hifadhi ya mazingira endelevu, kikao kilichofanyika
jijini Dodoma Juni 16, 2026.
Mkuu wa Biashara ya Serikali NMB Bi. Vicky Bishubo (Kushoto)
akizungumza wakati wa kikao na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa chenye lengo la kuimarisha
ushirikiano na kuweka mikakati ya pamoja ya hifadhi ya mazingira endelevu,
kikao kilichofanyika jijini Dodoma Juni 16, 2026.
****************
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa amewaomba wadau wa
maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kupanda miti ili
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.Amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa Benki ya NMB kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati ya pamoja ya hifadhi ya mazingira endelevu, kikao kimefanyika jijini Dodoma Juni 16, 2026.
Mhe. Kwagilwa alisema kuwa katika kufikia lengo la upandaji wa miti takriban bilioni mbili lililowekwa kupitia Dira 2050 zinahitajika nguvu za pamoja kati ya Serikali na wadau na kuendelea kuhamasisha jamii kupanda miti kwenye maeneo yao.
Alisema ni lazima kuunganisha nguvu za pamoja kushirikiana ili kuifanya nchi kuwa ya kijani kwani hata katika kaulimbiu iliyotumika kwenye Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu inasema ‘Dira 2050; Tuwajibike kukijanisha Tanzania’ ambayo inasisitiza umuhimu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
.jpg)
Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika
kikao cha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Reuben Kwagilwa na watendaji kutoka benki ya NMB chenye lengo la
kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati ya pamoja ya hifadhi ya mazingira
endelevu, kikao kilichofanyika jijini Dodoma Juni 16, 2026.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akiwa katika picha ya
pamoja na watendaji wa Benki ya NMB mara baada ya kufanya mazungumzo katika
kikao chenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati ya pamoja ya
hifadhi ya mazingira endelevu, kikao kilichofanyika jijini Dodoma Juni 16,
2026.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment