Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa William Samoei Ruto, anatarajiwa kuwasili nchini
leo, tarehe 04 Mei, 2026, kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.
Akiwa nchini, Rais Ruto atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na mwenyeji wake, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kabla ya
viongozi hao kuongoza mazungumzo rasmi ya pamoja kati ya ujumbe wa Tanzania na
Kenya, na kuzungumza na waandishi wa habari.
Mazungumzo hayo yataangazia jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kindugu na
kimkakati kati ya Tanzania na Kenya katika biashara, uwekezaji, miundombinu, usafirishaji
na maeneo mengine ya maslahi ya pamoja.
Viongozi hao pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini wa Hati za Makubaliano na
Mikataba ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya, pamoja na kushiriki Jukwaa la
Biashara litakalowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi zote mbili.
Aidha, siku ya Jumanne, tarehe 05 Mei, 2026, Rais Ruto anatarajiwa kuhutubia Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ziara yake. Siku
hiyohiyo baadaye, atarejea nchini Kenya baada ya kuhitimisha ziara yake nchini.
.jpg)
No comments:
Post a Comment