
Maadhimisho hayo yanabebwa na kaulimbiu isemayo, “Mazingira Bora ya Kazi Kisaikolojia ni Njia ya Kuimarisha Ustawi wa Wafanyakazi na Kujenga Taasisi Imara.”
Kilele cha maadhimisho hayo kimeongozwa na Deus Sangu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano.
Katika maonesho hayo, benki hiyo imekuwa ikiendelea kutoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wananchi wa Njombe na maeneo ya jirani, zikiwemo ufunguzi wa akaunti, elimu ya fedha pamoja na huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.
Wananchi wengi wamejitokeza kutembelea banda la benki hiyo kwa lengo la kujifunza na kunufaika na huduma zinazotolewa, hatua inayotajwa kusaidia kuongeza uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za kifedha.
Mbali na huduma hizo, CRDB Bank Plc pia imeendelea kutoa huduma za afya bure kwa wananchi kama sehemu ya mchango wake kwa jamii.
Benki hiyo ni mdhamini mkuu wa maadhimisho hayo muhimu, ambapo ushiriki wake unaakisi dhamira ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi sambamba na kulinda afya na usalama wa jamii.


















No comments:
Post a Comment