Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo itaanzisha utaratibu mpya wa kuingiza mafuta ya kupikia Tanzania Bara kutoka Zanzibar ili kuwezesha kufanyika kwa biashara halali ya mafuta na kuzuia mafuta ya magendo.
Amesema hayo Machi 17, 2026 katika Hoteli ya Madinat Al Bahr wakati wa Iftari iliyoandaliwa na TRA Zanzibar na kuhudhuriwa na watumishi wa TRA pamoja na Walipakodi huku mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema utaratibu huo unalenga kuingiza mafuta yanayowiana na upungufu uliopo ili kulinda viwanda vya ndani ambapo vitatolewa vibali maalum kwa waingizaji hao wa mafuta.
Amesema TRA inatambua mchango wa walipakodi wote wakiwemo waingizaji wa mafuta ndiyo maana imeandaa Iftari na kuwakutanisha pamoja na watumishi wa TRA.
Amesema TRA itaendelea kuwezesha biashara za walipakodi wote nchini na kuwapongeza watumishi wa TRA kwa kujituma na kuvuka malengo ya makusanyo kwa kila mwezi.





No comments:
Post a Comment