March 30, 2026

MBUNGE WA ZAMANI RAMADHANI BUNGARA 'BWEGE' AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini, Seleman Bungara almaarufu Bwege, amefariki dunia.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Bwege amefariki dunia mchana wa leo, Machi 30, 2026 akiwa anapatiwa matibabu hospitali iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu, Abbas Bungara amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa Bwege alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa huduma ya kusafisha damu (dialysis) kama kawaida yake, ndipo umauti ulipomfika.

Ameeleza kuwa msina upo Temeke jijini Dar es Salaam, nyumbani kwa marehemu.

No comments:

Post a Comment