January 27, 2026

WAZEE WASHIRIKIANA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII ZOEZI LA UPANDAJI MITI DODOMA

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipata mti nje ya jengo la Wizara leo tarehe 26 Januari, 2026 ikiwa zoezi la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira. 

Katibu Mkuu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akipata mti nje ya jengo la Wizara leo tarehe 26 Januari, 2026 ikiwa zoezi la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira. 
Mmoja wa Mzee Dijina Ndilito mti nje ya jengo la Wizara leo tarehe 26 Januari, 2026 ikiwa zoezi la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira. 

****************
Na Raymond Mushumbusi WMJJWM- Dodoma
Baadhi ya Wazee kutoka Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma wameshirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika zoezi la upandaji Miti kwa lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira.

Wakizungumza mara baada ya zoezi hilo wamempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake mahiri na thabiti katika kuliongoza taifa kwa misingi ya amani na utulivu.

"Tunampongeza Rais Samia kwa hatua yake ya kuitumia Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kuhamua kupanda Miti ili kuleta hamasa kwa watanzania katika kuyapenda na kuyatunza mazingira" wamesema Wazee hao.

Akiongoza zoezi hilo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi Januari 27, 2026 amesema lengo ni kuenzi maono ya Rais Samia la kutunza mazingira yanayotuzunguka.

Naibu Waziri Mahundi amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha kiongozi maono, mbunifu wake na namna anavyojali maslahi ya Taifa.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amesema Wizara imeshirikiana na kundi la Wazee kuwakilisha Makundi Maalum mengine yanayosimamiwa na Wizara katika zoezi hilo ambalo lina lengo kulinda na kutunza mazingira.

Zoezi la upandaji Miti mbele ya Ofisi ya Wizara Mtumba Jijini Dodoma limehusisha Kundi la Wazee Mkoa wa Dodoma, Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment