Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza leo
tarehe 26 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya watendaji
wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.(Picha na INEC).

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza leo
tarehe 26 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya watendaji
wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele ikiwa katika ufungaji wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka
Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya
Mbozi, mkoani Songwe wakifuatilia hotuba ya ufungaji mafunzo yao ya siku tatu.
Washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe wakifuatilia hotuba ya ufungaji mafunzo yao ya siku tatu.

Sehemu ya wajumbe wa Menejiment ya INEC ikiwa katika ufungaji wa mafunzo hayo.

********************
Na. Mwandishi Wetu, Iringa
Watendaji wa uchaguzi wametakiwa kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi na weledi ili kufanikisha uchaguzi mdogo wa ubunge
katika Jimbo la Peramiho na udiwani katika Kata ya Shiwinga unaotarajiwa
kufanyika tarehe 26 Februari, 2026.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk
Salim Mbarouk Mkoani Iringa leo tarehe 26 Januari, 2026 wakati akifunga mafunzo
ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 24 Januari,
2026.
“Ni matazamio ya Tume kwamba, baada ya
kupatiwa mafunzo haya, mtatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na weledi
mkizingatia ratiba ya utekelezaji ili kufanikisha uchaguzi mdogo wa ubunge
katika Jimbo la Peramiho na Udiwani katika Kata ya Shiwinga unaotarajiwa
kufanyika tarehe 26 Februari, 2026,” amesema Jaji Mbarouk.
Amesisitiza kuwa ili ufanisi uwepo ni muhimu
watendaji hao wazingatie sifa na uwezo wakati wa kuteua na kuajiri watendaji wa
vituo vya kupigia kura kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na
kuhesabu kura vituoni.
“Kuhusu ajira za kupata watendaji wa vituo,
tunayo imani kuwa mtateua na kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya
kazi hii muhimu……kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na
kuhesabu kura vituoni. Kazi ambayo inahitaji umahiri, umakini na weledi katika
kuitekeleza,” amesema Jaji Mbarouk.
Amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa
mafunzo ya watendaji wa vituo yanafanyika kwa ufanisi na weledi katika tarehe
zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga
kuwajengea uwezo ili waweze kufahamu majukumu yao na kuyatekeleza ipasavyo
wakati wa uchaguzi.
Jaji Mbarouk amewakumbusha watendaji hao kuwa
shughuli zote za uchaguzi zinaongozwa na Katiba, sheria, kanuni, maadili ya
uchaguzi na maelekezo ya Tume na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa kutenga sehemu
ya muda wao kusoma Katiba, sheria na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume
ili yawaongoze katika kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki.
Mafunzo hayo yamewahusisha Waratibu wa
Uchaguzi wa Mikoa ya Songwe na Ruvuma, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi
Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata,
Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ununuzi na Wahasibu.
Mada kadhaa ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na
Majukumu ya Watendaji wa Uchaguzi, Mambo Muhimu ya Kuzingatia, Uteuzi wa
Wagombea, Maadili na Kampeni za Uchaguzi, Wajibu na Majukumu ya Watendaji wa
Vituo na Utambulisho wa Mawakala wa Vyama vya Siasa, Taratibu za Upigaji Kura,
Taratibu za Kuhesabu Kura, Kujumlisha Kura na Kutangaza Matokeo, Fomu
Zinatotumika kwenye Uchaguzi, Mapokezi na Utunzaji wa Vifaa vya Uchaguzi na
Usimamizi wa Fedha za Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment