BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lkimemthibitisha kwa kauli moja Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwigulu, mtaalamu wa uchumi wa Tanzania na mwanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye amehudumu katika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwepo kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Sheria na Katiba na Waziri wa Fedha nafasi aliyoishika hadi anateuliwa kuwa Waziri Mkuu.
Aidha kwa upande wa siasa katika Chama chake cha Mapinduzi alipata kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa, na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.
Dkt. Mwigulu aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza 2010 akimtoa mtangulizi wake Mhe. Juma Hassan Killimbah na kuendelea kuchaguliwa na wananchi Iramba Magharibi katika chaguzi zote zinazofuata ukiwepo wa mwaka 2025.
Aliwahi kuwa miongoni mwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi walioonesha nia na kuchukua fomu za kuwania nafasi ya kugombea nafasi ya Rais kupitia Chama hicho.
Mwigulu anakuwa Waziri wa 12 tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania na anakua mrithi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa.
Waziri Mkuu Mteule, Dkt. Mwigulu Nchemba akitoa neno la shukurani baada ya kuthibitishwa na Bunge kwa Waziri Mkuu, Novemba 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Meteule, Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea maua kutoka kwa mtumishi wa Ofisi Binafsı ya Waziri Mkuu, Tecla Kilangi alipowasili kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma na kupokelewa na watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu, Novemba 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Mteule, Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonaz alipowasili kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 13, 2025. Kushoto ni Naibu Katibu, Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. James Kilabuko.Waziri Mkuu Mteule, Dkt. Mwigulu Nchemba akipongezwa na wabunge baada ya kuthibitishwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu, Novemba 13, 2025.

No comments:
Post a Comment