Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamemchagua Mhe. Mussa Azan Zungu kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungaano wa Tanzania kwa kura 378.
Akitangaza matokeo hayo baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo Bungeni leo, Katibu wa Bunge Ndg. Baraka Leonard alisema kura zilizopigwa zilikuwa 383 na kura zilizoharibika ni kura 3.
Wagombea waliopata kura moja kila mmoja ni Anitha Alfan Mkgaya wa chama cha NLD na Ndg. Ndonge Said Ndonge wa Chama cha AAFP huku wagombea wengine watatu ambao ni Ndg. Veronica Charles Tyeah wa NRA, Ndg. Christian Nyakita wa DP na Ndg. Amin Alfred Yango walipata kura sifuri kila mmoja.
Tayari Zungu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilala ameshaapisjwa kushika nafasi hiyo.
Aidha Bunge la 12 Zungu alikuwa Naibu Spika wa Bunge.

No comments:
Post a Comment