September 21, 2025

MWENYEKITI UWT MVOMERO AMWOMBEA KURA MAGALI NESTO, DKT. SAMIA NA SARA MSAFIRI ALLY

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Mvomero, Rachel Kingu, akimuombea kura za udiwani mgombea wa Kata ya Nyandira kupitia Chama Cha  Mapinduzi Bw. Magali Jamaica Nesto wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo katika kijiji cha Mwarazi, Mgeta Morogoro.
Mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Nyandira, tarafa ya Mgeta mkoani Morogoro, Magali Jamaica Nesto akihutubiwa waka wa kata huyo wakati wa uzinduzi wa kampeni katika kijiji cha Mwarazi.
*************
Na Mwandishi Wetu,Morogoro
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Mvomero, Rachel Kingu, amewaomba wananchi wa Kata ya Nyandira iliyopo Tarafa ya Mgeta wilayani Momvero, kumpa ridhaa Bw. Magali Jamaica Nesto, mgombea udiwani wa CCM, ili aweze kuwaletea maendeleo. 

Mama Kingu ametoa ombi hili kwenye uzinduzi wa kampeni za mgombea huyo uliofanyika katika Kijiji cha Mwarazi hivi karibuni.

Katika uzinduzi huo, Mama Kingu alitumia fursa hiyo kuwaombea kura za ndiyo mgombea Urais wa CCM,Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye mgombea Urais kupitia CCM, pamoja na Bi. Sara Msafiri Ally, mgombea Ubunge wa Jimbo la Mvomero. 

Alisisitiza umuhimu wa kura hizo kwa maendeleo ya taifa na wilaya.
Mama Kingu pia aliwahimiza wananchi kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu, akisisitiza kuwa amani ndiyo tunu pekee ya taifa. Aliwakumbusha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025.

Kwa upande wake, mgombea udiwani, Bw. Magali Jamaica Nesto, ameahidi kushirikiana na wananchi wa Mwarazi kuleta maendeleo endelevu endapo atachaguliwa. 

Alieleza baadhi ya ahadi zake ikiwemo kusaidia kufanikisha ukarabati wa barabara ya Langali, Bumu hadi Mwarazi kwa kiwango cha zege, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Mwarazi, kukamilisha ujenzi wa ofisi ya kijiji, na kupeleka vifaa vya umeme katika zahanati ya Mwarazi.

No comments:

Post a Comment