September 21, 2025

LORI LA MIZIGO LA ZAMBIA LA PATA AJALI MUFINDI IRINGA

Lori la Mizigo lenye namba za usajili za BCF 7439 lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Nchini Zambia likiwa limepata ajali katikati ya barabara kuu ya Iringa - Mbeya katika eneo la Mteremko wa Nyololo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa leo majira ya Saa 10 jioni Sepemba 21,2025. 

Askari wa Usalama Barabarani kutoka Jeshi la Polisi walifuika katika eneo la tukio kwa wakati na kutoa msaada ikiwa ni pamoja na kufungua njia ya dharula iliyopo eneo hilo ili magari yaweze kupita. 

Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa kuwa huenda ni hitilafu za kiufundi kwani lilisababisha kuyagonga magari mengine mawili ya mizigo yaliyokuwa yakipandisha mlima huo. 



 

No comments:

Post a Comment