September 03, 2025

KUNJE AMWAGA SERA MATOMBO MOROGORO, AHIDI KUFUGA MAMBA IKULU

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Wakulima AAFP Kunje Ngombale Mwiru Akiwa kwenye mwendelezo wa kampeni za Wagombea Urais, Wabunge na Madiwani katika Jimbo la Morogoro kusini kata ya Matombo amewahutubia wananchi wa eneo hilo na kunadi sera zake.

Ngombale Mwiru amesema ya kwamba kama akipata nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataanza kufuga mamba kwenye Ikulu yake.

Aidha Ngombale Mwiru aliweka wazi sababu ya kufuga mamba ni kitanzi cha mafisadi wote wa Nchi ambao watakuwa wanahujumu uchumi wa Nchi.








No comments:

Post a Comment