
Marehemu Abbas Hussein Mwinyi aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Fuoni Mkoa wa Magharib B Zanzibar aliyefariki juzi.
*************
Na Mwandishi wetu
Tume Hutru ya Taifa ya
Uchaguzi imetangaza kusitisha Shughuli za Uchaguzi Ubunge katika Jimbo la Fuoni
lililopo Mkoa wa Magharibi B visiwani Zanzibar kufuatia kifo cha Mgombea Ubunge
wa jimbo hilo kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
Taarifa iliyotolewa na Msimamizi
wa Uchaguzi Jimbo la Fuoni, Ndg. Miraji Mwadini Haji, amesema uamuzi huo
umefikiwa kwa masharti ya kifungu cha 71(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024.
Amesema Tume ilipokea barua yenye Kumb Na.
CCM/AKZ/U.30/22/VOL.XIV/109 ya tarehe 25 Septemba, 2025 kutoka kwa Naibu Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ikimtaarifu juu ya kifo cha Ndugu
Abass Ali Mwinyi aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Fuoni Wilaya ya
Magharibi B – Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Kutokana na kutokea kwa tukio
hilo, uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Fuoni, Wilaya ya Magharibi B -
Zanzibar umesitishwa kuanzia leo tarehe 25 Septemba, 2025,”. Imesema sehemu ya
taaifa hiyo.
Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 71(2) cha
Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume kwa
notisi itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali itapanga tarehe nyingine ya
uteuzi wa wagombea na taratibu za uchaguzi wa Ubunge katika jimbo husika
zitaanza upya.
“Hivyo, uteuzi kwa wagombea
wengine ambao walioteuliwa kihalali utabaki kama ulivyokuwa awali, isipokuwa
kama mgombea atajitoa,” imesema taarifa hiyo ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la
Fuoni.
Kufuatia hatua hiyo Tume
imesema hakutakuwa na kampeni kwa wagombea ubunge katika jimbo la Fuoni mpaka
baada ya uteuzi wa mgombea mwingine.
Kwa mujibu wa ratiba ya
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 iliyotolewa na Tume uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge
na Madiwani kwa Tanzania Bara umepangwa kufanyika Oktoba 29,2025.
Wananchi wa Jimbo la Fuoni
katika uchaguzi Mkuu huu sasa watalazimika kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Mwakilishi na udiwani pekee.
“KURAYAKO HAKIYAKO JITOKEZE
KUPIGA KURA"
No comments:
Post a Comment