Makamu
wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania
anayemaliza muda wake Mhe. Damptey Bediako Asare, mazungumzo yaliyofanyika
Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Agosti 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Damptey Bediako Asare, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Agosti 2025.
Makamu
wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi
zawadi Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe.
Damptey Bediako Asare, mara baada ya
mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Agosti
2025.
Makamu
wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na
Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Damptey
Bediako Asare, mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es
Salaam leo tarehe 29 Agosti 2025.
Makamu
wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika
picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda
wake Mhe. Damptey Bediako Asare, mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu
Jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Agosti 2025.
**************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Damptey
Bediako Asare, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Makamu
wa Rais amesema Tanzania na Ghana zimeendelea kunufaika na uhusiano uliopo wa
kihistoria ulioanza tangu kipindi cha utafutaji uhuru wa mataifa hayo ukichagizwa
na urafiki wa Baba wa Mataifa hayo, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere pamoja na Baba wa Taifa la Ghana hayati Kwame Nkurumah.
Amesema Tanzania inatambua mchango wa Jamhuri ya Ghana katika ukombozi wa
Mataifa ya Kusini mwa Afrika wakati wa kupigania uhuru.
Makamu wa Rais amesema mataifa
hayo mawili yameendeleza ushirikiano uliopo ambapo kwa sasa yamejikita zaidi
katika mahusiano ya kiuchumi. Ameongeza kwamba ni muhimu kuendelea kushirikiana
zaidi katika uwekezaji na biashara kupitia mpango wa Eneo Huru la Biashara Afrika
(AfCTFA). Aidha amesema ushirikiano zaidi unahitajika katika sekta mbalimbali
kama vile sekta ya madini, kilimo, utalii, TEHAMA, elimu na huduma za jamii. Amewakaribisha
wawekezaji kutoka nchini Ghana kuwekeza nchini Tanzania kupitia fursa nyingi
zilizopo.
Pia Makamu wa Rais ameipongeza
Ghana kwa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam
mwaka 2024. Amesema kupitia maonesho hayo, ushirikiano wa kiuchumi baina ya
mataifa hayo mawili umeongezeka na kutoa ujumbe kwa mataifa mengine umuhimu wa
kutoa kipaumbele katika kushirikiana mataifa ya Kiafrika yenyewe.
Halikadhalika Makamu wa Rais
ametoa salamu za pole kwa Serikali na Wananchi wa Ghana kufuatia ajali ya ndege
iliyotokea hivi karibuni na kusabibisha vifo vya watu nane ikiwemo Waziri wa Ulinzi
na Waziri wa Mazingira wa nchi hiyo. Amesema Tanzania inaungana na Jamhuri ya
Ghana katika kipindi cha majozi na kuwaombea marehemu waweze kupumzika kwa
amani.
Kwa upande Balozi wa Jamhuri
ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Damptey Bediako Asare ameishukuru
Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano aliopata kipindi chote alichohudumu kama
balozi nchini. Amewasilisha salamu za Rais wa Ghana Mheshimiwa John Mahama
ambazo amezitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan na Serikali kwa ujumla kwa kuendeleza ushirikiano na kuiunga
mkono Ghana katika nyanja mbalimbali hususani katika majukwaa ya kimataifa.
Amesema hayati, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere na hayati Kwame Nkurumah walitengeneza misingi ambayo nchi
nyingi barani Afrika zimeendelea kuitumia katika kudumisha amani na umoja. Balozi
Asare amesema ushirikiano huo unapaswa kuongezwa zaidi katika uchumi kwa
manufaa ya mataifa yote.
No comments:
Post a Comment