Nje kidogo ya jiji la Mwanza, mapinduzi ya kimya kimya yanatoke. Hakuna anayegundua. Kwenye shule iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF, wanafunzi wanafanya mambo ambayo hayakuzoeleka.Shule ya Sekondari Igogwe imejengwa na TASAF kwa majengo yote pamoja na vifaa vyake, kuanzia vyomba vya madaraka, ofisi ya walimu, mabweni na maabara na vifaa vyake.
Menejimenti ya TASAF imetembela shule hiyo kujionea maendeo yake na kukaribishwa na mawasisho na Power Point lililotoewa na mwanafunz wa Kidato cha Tatu Vella Francis kuhusu TASAF na kazi zake.
Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Athanas Manyika amesema shule hiyo ni miongzni mwa shule zinazofanya vizuri Zaidi katika Wilaya ya Ilemela kutokana na kuwa na vifaa vyote vinavyohitajika pamoja na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Katika maabda za Kemia na Fizikia, wanafunzi a madarasa tofauti, wakiwemo Baraka Charles na Ivan Shindika wa Kidato cha Nne na Isaya Wambura wa Kidato cha Tatu wanafanya majaribio mbalimbali wakishudiwa na viongozi TASAF waokuwa ametembelaa shuleni hapo.
Mwalimu Manyika anasema kuwa vifaa vilivyowekwa shuleni hapo ikiwa moja na maabara zenye vifaa vyote, mabweni na vyumba vya madaraka vinaleta mazingira mazuri na kujifunzia ka wanafunzi na mazingira bora ya walimu kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment