


Taarifa kutoka ofisi ya katibu mkuu wa chama hicho mwalimu Joseph misalaba ambaye kwa sasa anakaimu nafasi hiyo imeeleza kuwa mkutano huo wa saba unafanyika baada ya chama hicho kukamilisha chaguzi za ngazi za chini ambazo ni ngazi ya shule, ngazi ya wilaya na mkoa ambapo hivi sasa wanaelekea kwenye ngazi ya Taifa.
Taarifa hiyo iliyosasainiwa na Afisa habari na mahusiano wa chama hicho inazitaja nafasi zinazotarajia kugombewa kuwa ni rais wa chama, makamu wa rais wa chama, katibu mkuu, naibu katibu mkuu na mweka hazina wa chama hicho
Nafasi nyingine ni mwakilishi wa walimu wanawake, mwakilishi walimu walemavu, mwakilishi walimu vijana na wadhamini wa chama.
No comments:
Post a Comment