Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Augustine Vuma akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kamati hiyo kukagua jengo jipya la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo jijini Dodoma, Machi 13, 2025.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Augustine Vuma (mwenye shati jeupe-katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mshauri Elekezi, Blasius Venance baada ya Kamati hiyo kukagua jengo jipya la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo jijini Dodoma, Machi 13, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), kukagua jengo jipya la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo jijini Dodoma, Machi 13, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo (WMA) jijini Dodoma, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), kukagua jengo hilo, Machi 13, 2025. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Augustine Vuma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Alban Kihulla akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ilipozuru na kukagua jengo jipya la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo jijini Dodoma, Machi 13, 2025.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Prof. Eliza Mwakasangula akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ilipozuru na kukagua jengo jipya la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo jijini Dodoma, Machi 13, 2025
****************
Na
Mwandishi wetu, Dodoma
Mwenyekaiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe.
Augustine Vuma amesema kukamilika kwa Jengo la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo
(WMA), kutaongeza morali ya watumishi katika utendaji kazi hivyo kuboresha
zaidi huduma zake kwa wananchi.
Alikuwa
akizungumza na waandishi wa habari, Machi 13, 2025 baada ya Kamati hiyo kuzuru
na kujionea Jengo hilo jipya la kisasa lililojengwa na kampuni ya wakandarasi
wazawa ijulikanayo kama Ms. Mohammedi Builders Ltd kwa gharama ya shilingi za
kitanzania bilioni 6.1
“Ujio
wa Mradi huu unaamsha ari ya kufanya kazi kwa watumishi na ubunifu zaidi, jambo
ambalo tunaamini litaongeza tija kwa maana ya makusanyo ya Wakala, lakini pia
miradi itaenda kuwasaidia Watanzania kulindwa vizuri dhidi ya watu wasio
waaminifu ambao huwapunja wananchi kwenye vipimo mbalimbali,” amesema Mhe.
Vuma.
Aidha,
Mhe. Vuma ametoa pongezi kwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za
ujenzi wa jengo hilo.
Vilevile
ametoa pongezi kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo na
Menejimenti yote ya Wizara pamoja na Uongozi wa WMA kwa usimamizi mzuri
uliowezesha kufanikisha ujenzi husika.
Katika
hatua nyingine, Mhe. Vuma amempongeza Mkandarasi wa jengo hilo na kutoa rai kwa
Serikali pamoja na wadau wengine kuendelea kuwaamini wakandarasi wazawa
kutekeleza miradi mbalimbali ili fedha wanazolipwa ziendelee kubaki nchini na
kuchangia katika kukuza uchumi.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil
Abdallah, pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Samia kuwezesha ujenzi huo, pia
amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutawezesha kutimiza maono yake ya kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Dkt.
Hashil ameiahidi Kamati ya Bunge kutimiza maelekezo waliyoyatoa, hususan
yanayohusu Wizara na WMA kuutumia muda wa mwaka mmoja wa matazamio ya jengo kwa
kuhakikisha dosari ndogo ndogo zitakazojitokeza zinarekebishwa.
Akijibu
swali kutoka kwa mmoja wa waandishi wa habari kuhusu kuanza kutumika kwa jengo,
Katibu Mkuu amebainisha kuwa tayari makabidhiano yalikwishafanyika na kwamba
utaratibu wa kuhamisha watumishi umekwishaanza.
Ujenzi
wa Jengo hilo ulianza kutekelezwa Julai 2022 ambapo imeelezwa kuwa kukamilika
kwake kutaokoa matumizi ya kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kinalipwa kama
kodi ya pango kutokana na Wakala kutumia majengo ya kukodi kwa ajili ya Ofisi
yake kuu kwa muda mrefu.
Mradi
wa ujenzi wa jengo la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo umesimamiwa na Mshauri
Elekezi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Augustine Vuma (mwenye shati jeupe-katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mshauri Elekezi, Blasius Venance baada ya Kamati hiyo kukagua jengo jipya la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo jijini Dodoma, Machi 13, 2025.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakikagua jengo jipya la Ofisi Kuu ya Wakala wa Vipimo jijini Dodoma, Machi 13, 2025.
No comments:
Post a Comment