March 04, 2025

BENKI YA CRDB, UNDP ZAZINDUA PROGRAMU KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA KUFIKIA SOKO HURU LA AFRIKA (AfCTA)

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria kuzindua programu ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kushiriki fursa zilizopo katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP). Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa (wa pili kulia), Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (kulia) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Taasisi ya CRDB Bank Foundation (CBF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP), leo wamezindua mwongozo uliorahisishwa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini wenye fursa za kuwaunganisha na Soko Huru la Afrika (AfCTA) utakao wawaongezea uwezo na maarifa zaidi ili waweze kupanua biashara zao kote barani Afrika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambao baadaye ulifuatiwa na semina fupi kwa wajasiriali hao, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya CRDB, Naibu Waziri wa Viwanda, Mhe. Exaud Kagahe alisema “Serikali inajua faida za mkataba huu ndiyo maana Bunge liliidhinisha mnamo Septemba 2021, na hivyo kuifanya nchi yetu kustahiki kunufaika na Soko Huria la Afrika. Uamuzi huu wa serikali unalenga kufungua fursa kwa wajasiriamali wetu nje ya mipaka yetu ya kitaifa,”

Aliendelea kusema "Ili kuchukua fursa hizi kikamilifu, watu wetu lazima wawe na taarifa sahihi, maarifa muhimu, na ujasiri wa kuvuka mipaka kutafuta fursa hizi popote zinapojitokeza ndani ya mataifa 55 yetu Bara la Afrika. Kinachoendelea katika semina ya leo ni sehemu ya mikakati ya kuwawezesha wajasiriamali wetu kushindana na wenzao sokoni.”

Akielezea jukumu la CRDB Bank katika programu hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, TullyEsther Mwambapa alisema taasisi yake imejipanga kuhakikisha inatoa elimu ya fedha, mafunzo ya biashara na mitaji wezeshi itakayo wawezesha wajasiriamali kunufaika na Soko Huria la Afrika (AfCTA) linalokadiriwa kuwa na watu zaidi ya bilioni 1.4.

Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP), Mkurugenzi Mkaazi wa Shrika hilo, Shigeki Komatsubara alieleza fursa zinazoambatana na soko huru la AfCTA ikiwamo kuongezeka kwa biashara za ndani, kuvutia uwekezaji, na kuchochea mabadiliko ya kiuchumi hasa kwa wanawake wajasiriamali kote barani Afrika.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa (wa pili kulia), Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (kulia) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara wakipiga makofi wakati watazama video fupi katika hafla ya uzinduzi wa programu ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kushiriki fursa zilizopo katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe akizungumza na washiriki wa semina kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kushiriki fursa zilizopo katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation pamoja na UNDP.



Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa akizungumza na washiriki wa semina ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kushiriki fursa zilizopo katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation pamoja na UNDP.


Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara akizungumza na washiriki wa semina kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kushiriki fursa zilizopo katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation pamoja na UNDP.






Sehemu ya washiriki wa semina ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kushiriki fursa zilizopo katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation pamoja na UNDP.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa (wa tatu kulia), Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (wa pili kulia), Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara (wa tatu kushoto), Mkuu wa Uendeshaji CRDB Bank Foundation, Joyceline Makule (wapili kushoto), Mkuu wa Biashara changa Benki ya CRDB, Fadhil Bushagama pamoja na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo (wa kwanza kulia) wakiwa katika pic ha ya pamoja na washiriki wa semina ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati kushiriki fursa zilizopo katika Soko Huru la Afrika (AfCFTA) inayotekelezwa na CRDB Bank Foundation pamoja na UNDP.

No comments:

Post a Comment