February 01, 2025

WAPIGAKURA WAPYA LAKI NNE KUANDIKISHWA TANGA NA PWANI

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na wadau wa Uchgazi mkoa wa Tanga leo Februari 01, 2025 ikiwa ni maandalizi kuelekea zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mikao ya Pwani na mkoani Tanga  katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza na zoezi litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo wapiga kura wapya 431,016 wanatarajiwa kuandikishwa na zoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na wapiga kura 2,727,318. 

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani (Msf), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na wadau wa Uchgazi mkoa wa Pwani leo Februari 01, 2025 ikiwa ni maandalizi kuelekea zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mikao ya Pwani na mkoani Tanga  katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza na zoezi litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo wapiga kura wapya 431,016 wanatarajiwa kuandikishwa na zoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na wapiga kura 2,727,318. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndugu. Kailima R.K akiwasilisha mada wakati wa mkutano huo. 
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Tume na Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Tanga wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Uchaguzi wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na wadau wa Uchgazi mkoa wa Tanga leo Februari 01, 2025 ikiwa ni maandalizi kuelekea zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mikao ya Pwani na mkoani Tanga  katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza na zoezi litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025

Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria, Ndugu. Selemani Mtibora akiwasilisha mada katika mkutano wa Mkoani Pwani. 
Washiriki kutoka mkoa wa Pwani wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo. 
Na. Waandishi Wetu, Tanga na Pwani
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika mkoani Tanga na Pwani kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo wapiga kura wapya 431,016 wanatarajiwa kuandikishwa na zoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na wapiga kura 2,727,318.

Akifungua mkutano wa wadau mkoani Tanga, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa, Jacobs Mwambegele leo Januari 02, 2025 amesema mkoani Pwani zoezi hilo litafanyika kwa mkoa mzima na  mkoani Tanga  litajumuisha Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza.

“Leo tupo hapa Tanga na wenzetu wapo mkoa wa Pwani ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hii, ambapo zoezi litafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 13 Februari, 2025 na kukamilika tarehe 19 Februari, 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema Jaji Mwambegele.

Akifungua mkutano kama huo mkoani Pwani, Makamu Mwanyekiti wa Tume, Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk amesema tayari Tume imeshakamilisha zoezi hilo kwenye mikoa 25 na kwamba mikoa ya Lindi, Mtwara na sehemu ya Mkoa wa Ruvuma inakamilisha zoezi hilo Februari 03, 2025.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma, Singida, Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe na Ruvuma

mikoa miwili ya Mtwara na Lindi na sehemu ya mkoa wa Ruvuma kwenye halmashauri za Madaba, Namtumbo na Tunduru inatarajia kukamilisha zoezi hilo tarehe 03 Februari, 2025,” amesema.

Mada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndugu. Kailima R.K  ambayo ameiwasilisha mkoani Tanga na ambayo imewasilishwa kwa niaba yake Mkoani Pwani na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria, Ndugu. Selemani Mtibora imeeleza kuwa wapiga kura wapya 431,016 wanatarajiwa kuandikishwa na zoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na wapiga kura 2,727,318 sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 2,296,302 waliopo kwenye daftari katika mikoa hiyo.

“Idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha,” imesema sehemu ya nada hiyo.

No comments:

Post a Comment