Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-anayeshughulikia masuala ya Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Ridhiwani Kikwete amejitokeza katika Ofisi ya Kata ya Msoga, kwaajili ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
Kikwete ametumia fursa hiyo pia kuhamasisha wananchi wengine kujitokeza kujiandikisha au kuboresha taarifa zao ili haki hii muhimu ya kupiga kura isiwapite.
Zoezi hili limeanza Februari 13 na litaisha Februari 19, 2025 kwa mkoa wa Pwani na Tanga na hivyo kuwataka wananchi kutumia fursa hii kwa siku hizi zilizosalia.
Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi la kuweka taarifa zake sawa, Mh. Kikwete aliwahimiza wananchi kujitokea huku akisifu uharaka wa uhandikishaji na waandikaji walivyo na spidi ya kujiandikisha na ushirikiano wanaotoa kwa wanaokuja kujiandikisha.
Zoezi hili la uandikishaji pamoja na kuandikisha wapigakura wapya lakini linalenga kuboresha pia taarifa za wapiga kura wa zamani wakiwemo wale waliopoteza kadi zao.
No comments:
Post a Comment