January 14, 2025

WAZIRI MKUU ATOA WITO KWA VIONGOZI WA TAASISI ZA DINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya Jamaat Tanzania  kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam,  Januari 14, 2025
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya Jamaat Tanzania  kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam,  Januari 14, 2025
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya Jamaat Tanzania  kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam,  Januari 14, 2025
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na  Viongozi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya Jamaat Tanzania  baada ya mazungumzo kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam,  Januari 14, 2025. Kulia kwake ni Amir na Mbashiri Mkuu wa Ahmadiyya Musilim Jamaat Tanzania, Sheikh Khawaja Muzaffar Ahmad.
****************
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za dini nchini kuendelea kuwahamasisha waumini wake kudumisha amani na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Januari 14, 2025) alipokutana na viongozi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wapya wa jumuiya hiyo walikwenda kwa ajili ya kijitambulisha.

“…Fanyeni kazi kwa uhuru na wala msiwe na mashaka. Wahamasisheni Watanzania washiriki katika shughuli za kimaendeleo.” Pia amewashauri viongozi hao wabuni miradi ya kiuchumi kwani Tanzania kuna fursa nyingi za kimaendeleo.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza jumuiya hiyo kwa uwekezaji iliofanyika katika sekta mbalimbali zikiwemo afya na elimu ambapo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano katika jitihada zao hizo.

Amesema Serikali kwa upande wake inathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi mbalimbali za kidini nchini ikiwemo Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya, hivyo amewahakikishia ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake, Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya, Sheikh, Khawaja Muzaffar Ahmad ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri inayofanywa katika kuwahudumia Watanzania. “Nimeishi Tanzania kwa zaidi ya miaka 20, ni nchi nzuri hongereni kwa kazi nzuri mnazozifanya.”

Naye, Naibu Amiri, Sheikh Abdulrahman Mohammed 
ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi wake na amemuahidi Waziri Mkuu kwamba taasisi yao iko tayari kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji.

No comments:

Post a Comment