January 11, 2025

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AFRIKA KUHUSU KILIMO


Rais Yoweri Museveni wa Uganda  (wa nne kushoto) pamoja na viongozi wengene wakifuatilia hotuba ya Waziri Kassim Majaliwa aliyoitoa wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda,Januari 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya Wakuu wa Nchi  na Serikali wa Umoja wa  Afrika wakisikiliza wimbo wa taifa wa Uganda katika ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika  kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika uliofanyika  kwenye Kituo cha Mikutano cha  Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wenye mkutano huo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini mbele ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda  (kushoto) na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya kushuhudia  Tamasha la Kahawa Afrika. Africa Coffee Festival)  lililolenga kuhamasisha   uongezaji  thahamani katika mazao yanayolimwa Afrika likiwemo zao la kahawa. Tukio hilo lilifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda ambako alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Maalum wa  Wakuu wa Nchi na  Serikali wa Umoja wa  Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika, Januari 11, 2025.  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi  Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kufungua Mkutano Maalum wa  Wakuu wa Nchi  na Serikali wa Umoja wa  Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano  cha  Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi  Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kufungua Mkutano Maalum wa  Wakuu wa Nchi  na Serikali wa Umoja wa  Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano  cha  Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025.
*************
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema viongozi wa nchi za Afrika wameonesha matumaini makubwa na mikakati iliyowekwa na Tanzania katika kuzalisha mazao ya chakula yenye ubora hasa mpunga na mahindi.

Mheshimiwa Majaliwa amewahakikishia Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha masuala ya utafiti na kushirikisha sekta binafsi, taasisi za umma zinazojishughulisha na kilimo ili kuhakikisha nchi inakuwa tegemeo katika uzalishaji wa chakula barani Afrika.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Januari 11, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika wa kupitisha Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP 2026 - 2035) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala nchini Uganda. 

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imefarijika kusikia baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika akiwemo Mheshimiwa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wakiisifia Tanzania kwa kuzalisha mazao ya chakula yenye ubora na hasa mpunga na mahindi. “Haya ni mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo nchini.”

“Natamani watu washindane kwa ubora katika uzalishaji, mfano mchele wa kutoka Tanzania ni bora zaidi na gharama yake ipo chini, kuna wakati walitaka nizuie usije lakini nikawataka nao wajitahidi kushindana katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora.” Kauli ya Mheshimiwa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni aliyoitoa wakati akiwasilisha hotuba yake katika mkutano huo, inatoa fursa kwa mataifa mengine kununua mchele kutoka Tanzania.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania imeweka mkakati wa kuhakikisha inaendelea kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya ndani na kuuza  ziada nje. “Kwa sasa kilimo chetu si cha kujikimu bali ni cha kibiashara.”

Awali, Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza ili kuongeza tija na kukuza ajira hususan kwa vijana.

Ametoa mfano wa zao la kahawa, ambapo nchini Uganda kilo moja ya kahawa ghafi inauzwa dola mbili za Marekani, ambapo kahawa hiyo hiyo ikichakatwa bei inaongezeka na kuuzwa dola 40 za Marekani.

No comments:

Post a Comment